Polisi wa Malaysia wanamkamata Muisraeli aliyepanga mauaji ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i110064-polisi_wa_malaysia_wanamkamata_muisraeli_aliyepanga_mauaji_ya_kigaidi
Polisi ya Malaysia imemezuia operesheni ya mauaji ya kigaidi yaliyokuwa yamepangwa na shirika la ujasusi la Israel (Mossad) katika ardhi ya nchi hiyo.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Mar 30, 2024 03:50 UTC
  • Polisi wa Malaysia wanamkamata Muisraeli aliyepanga mauaji ya kigaidi

Polisi ya Malaysia imemezuia operesheni ya mauaji ya kigaidi yaliyokuwa yamepangwa na shirika la ujasusi la Israel (Mossad) katika ardhi ya nchi hiyo.

Mkuu wa Polisi ya Malaysia, Razaruddin Hussain amesema katika mkutano na waandishi wa habari  kwamba tarehe 27 mwezi huu wa Machi, mtu mwenye uraia wa Israel alikamatwa akiwa na bastola 6 na zaidi ya risasi 200.

Amesema mshukiwa huyo ana umri wa miaka 36, ​​na kwamba aliingia nchini Malaysia tarehe 12 mwezi huu kwa kutumia hati ya kusafiria ya Ufaransa.

Hussein amesema, imebainika kuwa mshukiwa huyo aliingia Malaysia "kwa kutumia hati ya kusafiria ya Ufaransa, na baada ya uchunguzi zaidi, mshukiwa huyo alikabidhi pasipoti yake ya Israel."

Taarifa ya polisi ya Malaysia imesema, awali Muisraeli aliyezuiliwa alidai kuwa "aliingia nchini humo kwa ajili ya kumfuatilia na kumuua raia wa Israel kutokana na mzozo wa kifamilia."

Hata hivyo vyombo vya usalama vya Malaysia haviamini madai ya mshukiwa huyo wa Israel, "na vinasema kuna uwezekano kwamba alikuwa na ajenda nyingine."  Mkuu wa polisi ya Malaysia ameongeza kuwa uchunguzi wa polisi imejikita kwenye uwezekano kwamba mshukiwa huyo alikuwa wakala wa shirika la ujasusi la Mossad.

Desemba 2022 mamlaka ya Malaysia ilifanikiwa kuzuia jaribio la Mossad la kuwateka nyara vijana wawili wa Kipalestina wanaoishi nchini humo.

Maajenti wa Mossad waliokamatwa awali nchini Malaysia

Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim hapo awali alisema kwamba amekuwa akikabiliwa na vitisho kwa sababu ya msimamo wake kuhusu vita vya Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kukataa kukemea Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na vilevile kuendeleza uhusiano wa Malaysia na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas).