-
Iran yakemea vikwazo vya Marekani dhidi ya majaji wa ICC
Dec 20, 2025 07:18Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeilaani vikali Marekani kwa kuwawekea vikwazo majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ikisema Washington inalinda waliotenda makosa makubwa ya jinai.
-
Kuipachika Venezuela lebo ya ugaidi; shutuma za kisiasa au kisingizio cha shambulio?
Dec 20, 2025 02:23Katika hatua yake ya hivi karibuni dhidi ya serikali ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Rais wa Marekani Donald Trump ameitangaza serikali hiyo kuwa ni ya kigaidi na ameamuru kuzuiwa meli zote za mafuta zinazoingia au kutoka nchini humo.
-
Guterres: Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya majaji wa ICC vinatia wasiwasi mkubwa
Dec 19, 2025 07:49Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya majaji wawili wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), akisisitiza jukumu la mahakama hiyo katika kuhakikisha haki kimataifa.
-
Assange awasilisha malalamiko dhidi ya Taasisi ya Nobel, asema ni chombo cha vita si amani
Dec 19, 2025 07:29Mwanzilishi wa WikiLeaks, Julian Assange, amewasilisha kesi ya jinai dhidi ya Taasisi ya Nobel huko Sweden kufuatia uamuzi wa taasisi hiyo wa kutoa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kiongozi wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado.
-
Ufaransa: Polisi wavamia nyumba na ofisi ya Waziri wa Utamaduni kwa madai ya ufisadi
Dec 19, 2025 06:46Polisi wa Ufaransa wamevamia nyumba ya Waziri wa Utamaduni, Rachida Dati, pamoja na makao makuu ya wizara na ofisi yake katika manispaa ya Paris, kufuatia kufunguliwa uchunguzi dhidi yake kuhusu tuhuma za ufisadi, utumiaji mbaya wa madaraka na ubadhirifu wa fedha za umma.
-
Kundi la "Hanzala" lavujisha taarifa nyeti na kudukua simu ya Naftali Bennett
Dec 19, 2025 06:30Mtandao wa al Mayadeen wa Lebanon umeripoti kuwa kundi la wadukuzi wa Iran, Hanzala, limedukua simu ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Naftali Bennett, katika operesheni iliyopelekea kuvujishwa mada nyeti na muhimu.
-
ICC: Vikwazo vya US ni 'hujuma' dhidi ya haki duniani
Dec 19, 2025 11:13Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imelaani vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya majaji wawili wa korti hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Kwa mara nyingine Pep Guardiola aikingia kifua Palestina
Dec 19, 2025 10:50Kocha maarufu wa timu ya ligi kuu ya Uingereza ya Mancester City kwa mara nyingine tena ameonesha uungwana na amechukua hatua ya kibinadamu ya kuwahami na kuwakingia kifua wananchi madhlumu wa Palestina.
-
Hizbullah ya Lebanon yalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Marekani
Dec 19, 2025 03:35Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani kwa maneno makali uhalifu na kitendo kiovu kilichofanywa na Mmarekani cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu, ikielezea tukio hilo kuwa la kichochezi linalotoa harufu mbaya ya chuki, na shambulio la wazi dhidi ya matakatifu zaidi ya Waislamu na maadili ya kidini na ya kibinadamu yanayowakilishwa na dini zote za mbinguni.
-
UN: Usafirishaji bidhaa duniani kote karibuni hivi utakuwa wa kasi na wa gharama nafuu zaidi
Dec 19, 2025 03:25Usafirishaji wa bidhaa kote duniani unatazamiwa kuwa wa gharama nafuu zaidi, unaofanyika kwa kasi zaidi na kwa urahisi mkubwa, kufuatia kupitishwa makubaliano mapya yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambayo yanahuisha nyaraka zinazotumika katika usafirishaji wa kimataifa.