-
Kitendo cha Waziri Kiongozi wa India kumvua Hijabu mwanamke hadharani chalaaniwa vikali
Dec 19, 2025 03:23Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International tawi la India, vyama vya siasa vya upinzani na wanaharakati mbali mbali wa ndani na nje ya nchi hiyo wamelaani vikali kitendo alichofanya Waziri Kiongozi wa Jimbo la Bihar cha kumvua niqabu hadharani daktari Muislamu katika hafla ya kiserikali iliyofanyika katika jimbo hilo.
-
Putin: Madai ya Magharibi kuwa Russia ni tishio ni urongo, upuuzi
Dec 18, 2025 10:25Rais wa Russia, Vladimir Putin amepuuzilia mbali madai ya Magharibi kuhusu shambulio 'tarajiwa' kutoka Moscow na kuyaeleza kuwa "uongo na upuuzi," akisisitiza kwamba kauli hizo zinatolewa kwa makusudi ili kushadidisha hali ya taharuki na wasiwasi katika eneo.
-
Maduro: Mpango wa Marekani wa kuigeuza Venezuela kuwa koloni lake 'kamwe hautatokea'
Dec 18, 2025 07:23Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesema kuwa matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu "kurejesha mikononi mwa nchi hiyo" ardhi na mafuta ya Venezuela yamefichua nia na sura halisi ya Marekani, na kusisitiza kuwa Washington haiwezi "kamwe" kuigeuza nchi hiyo ya Amerika Kusini kuwa "koloni" lake.
-
Polisi wa Uhispania wawafurusha mamia ya wahamiaji haramu katika mji wa Badalona
Dec 18, 2025 07:22Polisi nchini Uhispania Jumatano waliwafurusha mamia ya wahamiaji haramu waliokuwa wakiishi katika jengo la shule lililotelekezwa katika mji wa Badalona unaopakana na mji wa Barcelona kaskazini-mashariki mwa Uhispania.
-
Russia yafanya mashambulizi makubwa ya droni nchini Ukraine
Dec 18, 2025 02:46Russia imefanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani dhidi ya Ukraine kwa muda wa masaa kadhaa ambapo miripuko mikubwa imesikika huko Kyiv na miji mingine ya nchi humo.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Waislamu wachukue hatua baada ya Qur’ani Tukufu kuvunjiwa heshima Marekani
Dec 17, 2025 12:52Kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah nchini Yemen amelaani vikali kitendo cha hivi karibuni cha kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu kilichofanywa na mwanasiasa wa Marekani huku akiwataka Waislamu kote duniani kusimama imara kulinda matukufu yao.
-
Waziri Mkuu wa Australia amhutubu Muislamu aliyejitolea maisha yake: Wewe ni shujaa wa Australia
Dec 17, 2025 06:38Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ametembelea Hospitali ya St. George kusini mwa Sydney ili kumjulia hali Ahmed Al Ahmed, Mwislamu aliyehatarisha maisha yake kwa kumvamia na kumpokonya bunduki mmoja wa wahusika wa shambulio lililotokea kwenye Ufukwe wa Bondi na kusababisha vifo vya watu 15.
-
Mkuu wa White House akiri: Lengo hasa la kuzishambulia boti ni kumpindua Maduro
Dec 17, 2025 06:37Mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani White House Susie Wiles ametamka kuwa, mashambulizi ya jeshi la Marekani dhidi ya boti zinazodaiwa kuwa ni za madawa ya kulevya yanayofanywa katika eneo la Amerika Kusini yanalenga hatimaye kumpindua Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.
-
Lavrov: Iran haikuwahi kukanyaga makubaliano ya JCPOA
Dec 16, 2025 11:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesisitiza kwamba, Iran haijawahi kwenda kinyume na ahadi zake ndani ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, akisema kwamba Marekani ndiyo iliyoyachana na kuyatupa makubaliano hayo kwenye debe la taka.
-
Hungary: Mpango wa EU wa kuiba mali za Russia ni 'tangazo la vita'
Dec 16, 2025 06:30Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban ametahadharisha kuwa, hatua yoyote ya Umoja wa Ulaya ya kutwaa milki na fedha za Russia zilizozuiliwa bila idhini ya Budapest ni kukiuka sheria za Ulaya na itakuwa sawa na "tangazo la vita."