-
US yakiri kuwa Yemen ni tishio katika ulinzi wa anga baada ya F-16 kuvurumishiwa makombora
Nov 29, 2025 07:41Jeshi la Anga la Marekani limekiri kuwa ndege zake za kivita aina ya F-16 ziliandamwa na mashambulizi makali ya mitambo ya ulinzi wa anga ya Yemen wakati ndege hizo zilipokiuka anga ya nchi hiyo.
-
Baraza la Waislamu Ufaransa latoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu ujasusi dhidi ya Waislamu kwa niaba ya Israel
Nov 28, 2025 23:54Baraza la Waislamu la Ufaransa limetoa wito kwa serikali kuanzisha uchunguzi kuhusu madai kwamba watu wawili walikusanya taarifa kuhusu Waislamu nchini Ufaransa na kuzikabidhi kwa shirika la ujasusi la Israel.
-
Kwa kupiga marufuku shughuli za kundi la 'Palestine Action', Uingereza ni mtetezi kweli wa uhuru wa kutoa maoni?
Nov 28, 2025 23:12Kundi linalolitetea taifa madhulumu la Palestina nchini Uingereza liitwalo 'Palestine Action' limesema, kupigwa marufuku uendeshaji wa shughuli zake na serikali ya London ni hatua ya kidikteta.
-
Maelfu ya wafanyakazi waandamana Ireland kulaani jinai za Israel
Nov 28, 2025 08:14Maelfu ya wafanyakazi wameandamana nchini Ireland kulaani kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina.
-
Makumi waaga dunia kwa mafuriko Indonesia, Thailand na Malaysia
Nov 28, 2025 08:10Kwa akali watu 250 wamefariki dunia katika mataifa ya Indonesia, Thailand na Malaysia kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko na maporomoko ya ardhi.
-
Trump avunja rekodi ya kuwa kiongozi anayechukiza zaidi katika historia ya Marekani
Nov 28, 2025 03:02Marais wa Marekani kwa kawaida huwa wanakumbwa na janga la kupungua umaarufu wa muda mfupi baada ya kuingia madarakani. Lakini kwa mujibu wa The Economist, hakuna rais katika miongo ya hivi karibuni ambaye amepitia janga la kupungua mno umaarufu wake kama lilivyomkuba janga hilo Donald Trump.
-
Putin: Pendekezo la Marekani linaweza kuwa msingi wa makubaliano ya amani ya siku zijazo
Nov 28, 2025 03:02Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, vipengele vya rasimu ya amani vilivyojadiliwa hivi karibuni na Marekani na Ukraine vinaweza kutumika kama msingi wa makubaliano ya siku zijazo ya kukomesha vita nchini Ukraine.
-
Iran yawaonya mahasimu kuhusu mbinu za mabavu na mashinikizo
Nov 27, 2025 08:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa onyo kali kwa mahasimu wa Jamhuri ya Kiislamu akiwataka waache mwenendo wa mabavu na mashinikizo ya kupita kiasi dhidi ya taifa hili.
-
Marekani ina kiwewe cha kudukuliwa na Iran kombora lake la GBU-39B
Nov 27, 2025 02:30Marekani imeingiwa na kiwewe kikubwa cha kudukuliwa kombora lake la GBU-39B lililopatikana nchini Lebanon na kuziruhusu nchi zisizo rafiki kwake hasa Iran na Russia kupata teknolojia iliyotumika kwenye kombora hilo la kisasa na kuwa hatari kwa Marekani na utawala wa Kizayuni.
-
Mkutano wa Luanda: Ulaya na Afrika zakubaliana kushirikiana zaidi
Nov 26, 2025 22:58Mataifa ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika yamesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu mwishoni mwa mkutano wao wa siku mbili katika mji mkuu wa Angola, Luanda.