Nov 16, 2023 04:12 UTC
  • Wamadagascar washiriki uchaguzi wa rais uliosusiwa na upinzani

Wananchi wa Madagascar hii leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kushiriki uchagujzi wa rais ambao umesusiwa na upinzani.

Marc Ravalomanana ni mmoja wa marais wawili wa zamani waliojiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho, huku wakitoa mwito wa kwa wafuasi wao kususia uchaguzi huo.

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo wanasisitiza kuwa, Rais wa sasa Andry Rajoelina hana ustahiki wa kugombea urais katika uchaguzi huo.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Rajoelina mwenye miaka 49 alijiuzulu wadhifa wake huo mwezi Septemba mwaka huu kwa mujibu wa katiba ili kugombea tena urais.

Uchaguzi wa leo unafanyika wiki moja baada ya Spika wa Bunge la nchi hiyo kutoa wito wa kusimamishwa zoezi hilo la kidemokrasia. Christine Razanamahasoa alisema: "Mchakato wa uchaguzi lazima uzingatie viwango vya kimataifa." 

Raoajoelina (kushoto) na Marc Ravalomanana

Wagombea 11 kati ya 13 wa upinzani wamekuwa wakiongoza maandamano ya karibu kila siku mjini Antananarivo kwa zaidi ya mwezi mmoja, wakipinga kile walichokiita "mapinduzi ya kitaasisi" ambayo yanampendelea rais aliyeko madarakani.

Jana Jumatano, serikali ya kisiwa hicho cha kusini mashariki mwa Afrika katika Habari Hindi ilitangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku, kuelekea uchaguzi wa leo.

Watu milioni 11 kati ya idadi jumla ya watu milioni 30 wa Madagacar wamesajiliwa na kutimiza masharti ya kushiriki uchaguzi.

Tags