- 
        
            
            Madagascar yamvua uraia aliyekuwa rais wa nchi hiyo Rajoelina
Oct 25, 2025 14:51Rais wa zamani wa Madagascar, Andry Rajoelina, amevuliwa uraia wake baada ya kuikimbia nchi hiyo mapema mwezi huu kufuatia maandamano makubwa yaliyoongozwa na vijana dhidi ya utawala wake.
 - 
        
            
            Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Madagascar amteua mfanyabiashara kuwa waziri mkuu mpya
Oct 21, 2025 07:01Rais wa mpito wa Madagascar Kanali Michael Randrianirina amemteua mfanyabiashara Herintsalama Rajaonarivelo kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo na kumuapisha katika hafla rasmi iliyofanyika kwenye Ikulu ya Jimbo la Iavoloha.
 - 
        
            
            AU yaisimamishia uanachama Madagascar kufuatia mapinduzi ya kijeshi
Oct 16, 2025 06:24Umoja wa Afrika umetengaza kuisimamishia unachama Madagascar "hadi utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa" baada ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Andry Rajoelina.
 - 
        
            
            Mahakama ya Madagascar "yamwita" kanali wa jeshi akachukue uongozi na kuitisha uchaguzi
Oct 15, 2025 06:02Mahakama ya Juu ya Katiba ya Madagascar jana Jumanne "ilimwita" kamanda wa Kituo cha Uendeshaji cha Wafanyakazi wa Jeshi (CAPSAT) Kanali Michael Randrianirina "akatekeleze kazi za mkuu wa nchi."
 - 
        
            
            Rajoelina atangaza kulivunja Bunge la Madagascar akiwa 'mafichoni'
Oct 15, 2025 02:34Rais wa Madagascar anayesakamwa na mashinikizo ya kujiuzulu, Andry Rajoelina ametangaza kulivunja Bunge kufuatia wiki kadhaa za maandamano dhidi ya serikali yake kote nchini, akisema ni muhimu kurejesha utulivu na kutoa nafasi kwa vijana.
 - 
        
            
            Wanajeshi wa Madagascar waungana na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu
Oct 12, 2025 05:25Baadhi ya makundi ya wanajeshi wa Madagascar yamekaidi amri na kuungana na maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali, ambao wamekusanyika katika mji mkuu, Antananarivo, huku maandamano ya kupinga utawala wa Rais Andry Rajoelina yakizidi kupamba moto.
 - 
        
            
            Rais wa Madagascar afanya mazungumzo licha ya waandamanaji kususia
Oct 09, 2025 07:13Rais Andry Rajoelina wa Madagascar jana aliyaalika makundi na asasi kadhaa za kiraia kwa ajili ya mazungumzo katika ikuu ya Rais.
 - 
        
            
            Rais wa Madagascar amteua jenerali wa jeshi kuwa Waziri Mkuu mpya
Oct 07, 2025 03:11Rais Andriy Rajoelina wa Madagascar amemteua Jenerali Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo wiki moja baada ya kulivunja baraza la mawaziri kufuatia maandamano ya wananchi ya siku kadhaa.
 - 
        
            
            Maandamano yashtadi Madagascar huku Rais akishinikizwa kujiuzulu
Oct 02, 2025 07:55Mitaa mbali ya Madagascar jana Jumatano ilishuhudia maandamano ya wananchi wanaoshinikiza kujiuzulu raia wa nchi hiyo. Polisi ya nchi hiyo kwa upande wake walichukua hatua za kuzuia kuibuka ghasia katika maandamano hayo.
 - 
        
            
            Rais wa Madagascar avunja serikali sambamba na watu wasiopungua 22 kuuawa katika maandamano
Sep 30, 2025 07:05Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameivunja serikali yake siku ya Jumatatu kutokana na kupamba moto maandamano ya upinzani yanayoongozwa na vijana ya kulalamikia uhaba mkubwa wa maji na umeme, mgogoro ambao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa umesababisha vifo vya watu wasiopungua 22 na kujeruhiwa zaidi ya 100 katika kile kinachotajwa kama changamoto kubwa zaidi kuukabili utawala wake baada ya miaka kadhaa.