Maandamano yashtadi Madagascar huku Rais akishinikizwa kujiuzulu
Mitaa mbali ya Madagascar jana Jumatano ilishuhudia maandamano ya wananchi wanaoshinikiza kujiuzulu raia wa nchi hiyo. Polisi ya nchi hiyo kwa upande wake walichukua hatua za kuzuia kuibuka ghasia katika maandamano hayo.
Askari usalama waliweka vizuizi katikati ya mji wa Antananarivo ili kuwazuia waandamanaji kufika katika eneo kwa jina la Maidani ya Demokrasia. Polisi walinyunyiza gesi za kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji. Waaandamaji na waandishi wa habari wamelaani mashambulizi ya askari usalama dhidi ya uhuru wao wa kujieleza.
Maandamano hayo yanayoongozwa na Gen-Z yamekuwa yakiendelea huko Madagascar tangu Alhamisi iliyopita na yalichochewa na ghadhabu za wananchi wanaolalamikia uhaba wa maji na umeme.
Jumatatu wiki hii Rais Andry Rajoelina wa nchi hiyo alifuta serikali katika jaribio lililofeli la kuwatuliza waandamanaji.
Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa mgogoro wa Madagascar umesababisha vifo vya watu wasiopungua 22 na kujeruhiwa zaidi ya 100 katika kile kinachotajwa kama changamoto kubwa zaidi kuukabili utawala wa Rajoelina baada ya miaka kadhaa.