Rais wa Madagascar amteua jenerali wa jeshi kuwa Waziri Mkuu mpya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i131680-rais_wa_madagascar_amteua_jenerali_wa_jeshi_kuwa_waziri_mkuu_mpya
Rais Andriy Rajoelina wa Madagascar amemteua Jenerali Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo wiki moja baada ya kulivunja baraza la mawaziri kufuatia maandamano ya wananchi ya siku kadhaa.
(last modified 2025-10-07T03:11:34+00:00 )
Oct 07, 2025 03:11 UTC
  • Rais wa Madagascar amteua jenerali wa jeshi kuwa Waziri Mkuu mpya

Rais Andriy Rajoelina wa Madagascar amemteua Jenerali Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo wiki moja baada ya kulivunja baraza la mawaziri kufuatia maandamano ya wananchi ya siku kadhaa.

Waziri Mkuu mpya wa Madagascar ambaye ametoka katika kikosi cha uongozi jeshini, alihitimu katika Chuo cha Kijeshi cha Antsirabe mwaka 1991 kabla ya kupata mafunzo ya upili ya jeshi nchini Ufaransa. 

Maandamano nchini Madagascar ambayo yalikuwa yameingia katika wiki ya tatu yalisababishwa na kutoridhishwa wananchi na kukatika pakubwa huduma za umeme na maji nchini humo. 

Maandamano hayo kwa kiasi kikubwa yaliongozwa na wanafunzi na wanaharakti vijana. 

Maandamano yalishuhudiwa tena jana nchini Madagascar huku askari usalama walijaribu kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji. Wananchi Madagascar wanashikiza kujiuzulu Rais Rajoelina. 

Akihutubia siku ya Jumamosi, Rais wa Madagascar alieleza kuwa yupo tayari kusikiliza matakwa ya wananchi hata hivyo alipuuzilia mbali wito wa kujiuzulu. Amewatuhumu mahasimu wake kuwa wana lengo la kuipindua serikali yake. 

Akizungumza jana na wawakilishi wa jumuiya za kiraia, Rais wa Madagascar amesema kuwa hana nia ya kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu.