Ruto: Watu wasiofahamika wanaoibua ghasia wanatishia demokrasia ya Kenya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i114328-ruto_watu_wasiofahamika_wanaoibua_ghasia_wanatishia_demokrasia_ya_kenya
Rais William Ruto wa Kenya amewatuhumu watu wasiojulikana wanaoibua machafuko kuwa wanatishia demkrasia ya nchi hiyo kufuatia maandamano yanayoikumba nchi hiyo.
(last modified 2024-07-21T23:01:10+00:00 )
Jul 21, 2024 23:01 UTC
  • Ruto: Watu wasiofahamika wanaoibua ghasia wanatishia demokrasia ya Kenya

Rais William Ruto wa Kenya amewatuhumu watu wasiojulikana wanaoibua machafuko kuwa wanatishia demkrasia ya nchi hiyo kufuatia maandamano yanayoikumba nchi hiyo.

Rais wa Kenya amesem serikali yake haitasalimisha demokrasia ya nchi hiyo kwa watu wasiofahamika wala kutambulika ambao wanafadhili ghasia na machafuko huko Kenya. 

Rais wa Kenya ametamka haya jana huku maandamano zaidi yakipangwa kufanyika kesho Jumanne wiki hii baada ya Ruto kutangaza sehemu ya baraza lake la mawaziri huku akiwarejesha mawaziri sita wa hapo awali. 

Hatua ya Rais wa Kenya ya kuwarejesha nyadhifani mawaziri sita imeibua duru nyingine ya maandamano, huku waratibu wa maandamano hayo wakimtuhumu rais William Ruto kwa kufanya kosa la kuwateua tena mawaziri hao ambao waliisimamia vibaya nchi na kusababisha kushuhudiwa maandamano makubwa huko Kenya hivi karibuni yaliyopelekea kuuliwa zaidi ya watu 50.

Maandamano Kenya ya G-Z

Rais Ruto amesema kuwa maandamano yanayoshuhudiwa takriban kila wiki huko Kenya yanafadhiliwa na watu wasiofahamika wenye nia ya kuliyumbisha taifa hilo la Afrika Mashariki.  

Vijana wa Gen-Z huko Kenya walianza kufanya maandamano mwezi uliopita kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 ambao ungechangia kuongezeka viwango vya ushuru; lakini sasa yamebadilika na kuwa maandamano ya kukosoa utawala wa Rais Ruto.