Watu wasiojulikana wajaribu kumuua kwa sumu Waziri wa Sheria wa DR Congo
(last modified Sun, 08 Sep 2024 06:33:28 GMT )
Sep 08, 2024 06:33 UTC
  • Watu wasiojulikana wajaribu kumuua kwa sumu Waziri wa Sheria wa DR Congo

Watu wasiojulikana wamejaribu kumuua kwa sumu Waziri wa Sheria na Mlinzi wa Mihuri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Constant Mutamba.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Actualite, jaribio hilo la mauaji kwa sumu limejiri wakati ambao ndani, waziri Mutamba ameanzisha mageuzi ya mfumo wa mahakama nchini DRC, ambao unatishia kuwafukuza kazi majaji wanaoshukiwa kuhusika na ufisadi.

Tovuti hiyo imeongeza kuwa, "Vipimo vilivyofanywa vimebaini kuwepo sumu katika mwili wa Mutamba, imeripoti tovuti hiyo na kuwa hatua kali zinachukuliwa kumtunza waziri."

Vyombo vya habari havikutoa maelezo kuhusu hali ya Mutamba au mahali alipo.

Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Sheria ya DRC, ofisi ya waziri ilivunjwa usiku wa Septemba 2. Baadaye, wataalamu waligundua chembechembe za unga mweupe katika ofisi yenyewe na kwenye korido inayoelekea huko. Chemechembe za sumu pia zilipatikana kwenye jokofu linalotumiwa na waziri.