Sep 17, 2024 08:20 UTC
  • Kuondoka kabisa wanajeshi wa Marekani nchini Niger

Jeshi la Marekani limetangaza kuwaondoa wanajeshi wake wote katika ardhi ya Niger.

Kamandi ya jeshi la Marekani imetangaza katika taarifa kwamba mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Niger umekamilika kabisa, na kwamba uondoaji wa wanajeshi na zana za kijeshi za Marekani katika Kambi ya 101 ya Wanahewa huko Niamey mnamo Julai 7 na kujiondoa kwenye Kambi ya 201 ya Wanahewa huko Agadez mnamo Agosti 5 mwaka huu 2024 umekamilika.

Uondoaji wa vikosi vya jeshi la Marekani kutoka Niger umekamilika

Sabrina Singh naibu msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani (Pentagon) pia alitangaza siku ya Jumatatu katika taarifa kwamba; uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Niger ni mdogo sana na kwamba sasa wanalinda tu usalama katika ubalozi wa Marekani nchini humo.

Mwezi Aprili mwaka jana, serikali ya kijeshi ya Niger iliiamuru Marekani kuwaondoa wanajeshi 1,000 nchini humo, jambo ambalo lilikuwa aibu kubwa kwa Washington.

Tags