Ripoti yabaini namna Waisraeli wanavyopora figo za Wakenya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i125202-ripoti_yabaini_namna_waisraeli_wanavyopora_figo_za_wakenya
Hospitali moja kibinafsi nchini Kenya yenye matawi kadhaa Afrika Mashariki, inachunguzwa na serikali ya Kenya baada ya kubainika kuwa inauhusika katika mtandao wa ulanguzi wa viungo vya binadamu ambavyo vinauziwa watu kutoka nje ya nchi hiyo wakiwemo Waisraeli.
(last modified 2025-04-15T06:43:07+00:00 )
Apr 15, 2025 06:43 UTC
  • Ripoti yabaini namna Waisraeli wanavyopora figo za Wakenya

Hospitali moja kibinafsi nchini Kenya yenye matawi kadhaa Afrika Mashariki, inachunguzwa na serikali ya Kenya baada ya kubainika kuwa inauhusika katika mtandao wa ulanguzi wa viungo vya binadamu ambavyo vinauziwa watu kutoka nje ya nchi hiyo wakiwemo Waisraeli.

 Uchunguzi huo unahusisha ripoti  upandikizaji wa figo usio wa kimaadili na ukiukaji wa sheria za afya.

Kulingana na ripoti, mtandao wa kimataifa unatumia watu maskini na wasiojiweza nchini Kenya kuuza figo zao kwa wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali za dunia, hasa raia wa utawala haramu wa Israel.

Ripoti hiyo ya kushitua, iliyotolewa na Huduma ya Kitaifa ya Damu na Upandikizaji Viungo (KBTTS), inaonesha hali ya kutisha ya uwepo wa mtandao wa ulanguzi wa viungo.

Mtandao huo wa siri unaonekana kuvuka mipaka, kutumia mianya ya kisheria, na kuvunja maadili ya kitabibu kwa ajili ya faida ya kifedha, wakisingizia kuwa wanaokoa maisha.

Kamati maalum ya wachunguzi 12 iliyoteuliwa na Dkt. Maurice Wakwabubi, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Damu na Upandikizaji Viungo (KBTTS), imefichua kile kinachoonekana kuwa ni mtandao mkubwa wa ulanguzi wa viungo unaohusishwa na Kituo cha Uzazi na Upandikizaji cha Mediheal kilichopo Eldoret, magharibi mwa Kenya.

Ripoti hiyo, iliyopewa jina "Ujumbe wa Ukweli katika Hospitali ya Mediheal – Ripoti ya Eldoret", inaeleza dosari kubwa katika upandikizaji wa figo uliofanywa tangu mwaka 2018.

Kamati hiyo ilichunguza visa 372 vya upandikizaji wa figo vilivyofanyika hospitalini hapo. Ingawa kiwango cha vifo kilikuwa asilimia nne—ambacho kwa mtazamo wa haraka kinaweza kuonekana kuwa cha kawaida—ni mifumo iliyo nyuma ya takwimu hizo ndiyo iliyozua mashaka.

Dkt. Jonathan Wala, mkuu wa Chama cha Madaktari wa Figo nchini Kenya, amewatibu wagonjwa kadhaa waliorejea na matatizo baada ya upasuaji.  Amesema kuna ripoti za Waisraeli waliokuja Kenya wakiwa na figo zilizokufa kabisa kwa ajili ya kupata figo za Wakenya masikini.

Madaktari wenzake wametoa tahadhari kwa mamlaka za Kenya kuhusu upandikizaji usio wa kimaadili unaofanyika katika Hospitali ya Mediheal.

Taarifa zinasema raia wa kigeni wanalipa hadi  dola 200,000 kwa figo moja katika hali ambayo Mkenya ambaye anahadaiwa kuuza figo yake analipwa dola 6000 tu.