Jeshi la Msumbiji: Uasi katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo Delgado umemalizika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i125606-jeshi_la_msumbiji_uasi_katika_mkoa_wenye_utajiri_wa_gesi_wa_cabo_delgado_umemalizika
Jeshi la Msumbiji limetangaza kuwa limedhibiti kambi za mwisho za mafunzo zilizokuwa zikitumiwa na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado, ikiwa ni ishara ya kile wanachokitaja maafisa wa jeshi hilo kuwa ni kumalizika kwa uasi wa miaka mingi katika eneo hilo lenye utajiri wa maliasili ya gesi.
(last modified 2025-12-30T05:43:50+00:00 )
Apr 25, 2025 06:42 UTC
  • Jeshi la Msumbiji: Uasi katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo Delgado umemalizika

Jeshi la Msumbiji limetangaza kuwa limedhibiti kambi za mwisho za mafunzo zilizokuwa zikitumiwa na waasi katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado, ikiwa ni ishara ya kile wanachokitaja maafisa wa jeshi hilo kuwa ni kumalizika kwa uasi wa miaka mingi katika eneo hilo lenye utajiri wa maliasili ya gesi.

Mkuu wa Intelijensia ya jeshi la Msumbiji Ricardo Macuvele amesema operesheni hiyo imefanikiwa kutokana na mchango wa vikosi vya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC vilivyoko nchini humo, ambavyo vimetoa mchango mkubwa katika kuwashinda waasi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi jana Alkhamisi Macuvele aliipongeza pia nchi jirani ya Zambia akisema nayo pia iliisaidia sana Msumbiji kulikomboa eneo la Cabo Delgado kutoka kwenye udhibiti wa magaidi.

Kiwango kikubwa cha gesi asilia kiligunduliwa katika eneo la Cabo Delgado mwaka 2010. Wapiganaji wanaohusishwa na kundi la kigaidi la DAESH walianzisha uasi mkoani humo mwama 2017 na kusitisha uchimbaji wa gesi hiyo. Imeelezwa kuwa watu wapatao 5,800 wameuawa katika machafuko na mapigano yaliyosababishwa na kundi hilo.

Kampuni ya TotalEnergies, ambayo ilisitisha mradi huo mkubwa wa uchimbaji gesi baada ya mashambulizi ya 2021 ambapo watu kadhaa waliuawa, imetangaza kuwa mradi huo utaanza tena mwaka huu pale "amani na usalama" vitakaporejea huko Cabo Delgado.../