ECOWAS yapinga mpango wa mpito wa kijeshi wa Guinea-Bissau
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i134350-ecowas_yapinga_mpango_wa_mpito_wa_kijeshi_wa_guinea_bissau
Viongozi wa Afrika Magharibi wamepinga mpango wa mpito uliotangazwa na watawala wa kijeshi wa Guinea-Bissau, badala yake wametaka kurejea haraka kwa utaratibu wa kikatiba. na kuonya kuhusu vikwazo vinavyolengwa dhidi ya wale wanaozuia mchakato huo.
(last modified 2025-12-16T02:51:05+00:00 )
Dec 16, 2025 02:51 UTC
  • ECOWAS yapinga mpango wa mpito wa kijeshi wa Guinea-Bissau

Viongozi wa Afrika Magharibi wamepinga mpango wa mpito uliotangazwa na watawala wa kijeshi wa Guinea-Bissau, badala yake wametaka kurejea haraka kwa utaratibu wa kikatiba. na kuonya kuhusu vikwazo vinavyolengwa dhidi ya wale wanaozuia mchakato huo.

Viongozi wa Afrika Magharibi pia wametahadharisha kuwa vikwazo kwa wale watakaozuia kurejea kwa mchakato huo. 

Viongozi wa Afrika Magharibi wameeleza haya katika Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ulioanza rasmi siku yaJumapili mjini Abuja, Nigeria, ukikusanya viongozi wa kikanda kujadili masuala nyeti yanayoathiri eneo la Afrika Magharibi.

Katika hotuba ya ufunguzi, Julius Maada Bio Rais wa Sierra Leone ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya ECOWAS ametahadharisha kuwa kuibuka upya kwa mabadiliko ya serikali kinyume na katiba ni tishio kubwa kwa utulivu wa kikanda.

Amesema,wasanifu wa ECOWAS wanatambua kuwa demokrasia haiwezi kutenganishwa na amani, haki na maendeleo. " Leo hii, utaratibu  wa kidemokrasia unajaribiwa. Kuibuka upya kwa mabadiliko ya serikali kinyume na katiba kunatishia uthabiti wetu wa kikanda, unadhoofisha haki za raia wetu, na kudhoofisha mustakabali wetu wa pamoja," amesema Mwenyekiti wa Kamisheni ya ECOWAS. 

Naye Kashin Shettima Makamu wa Rais wa Nigeria ambaye alimwakilisha Rais Bola Tinubu katika mkutano huo amewataka viongozi kufungamana na ahadi zao kwa amani na utulivu wa kikanda.