Watu 10 wauawa katika mapigano mapya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41467-watu_10_wauawa_katika_mapigano_mapya_kaskazini_mashariki_mwa_nigeria.
Kwa akali watu 10 wameripotiwa kuuawa katika shambulizi la watu wenye silaha kaskazini mashariki mwa Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 10, 2018 11:46 UTC
  • Watu 10 wauawa katika mapigano mapya kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Kwa akali watu 10 wameripotiwa kuuawa katika shambulizi la watu wenye silaha kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Shambulizi hilo limetokea katika eneo la Daffo jimbo la Plateau nchini humo ambapo watu wengine 10 pia wamejeruhiwa. Viongozi wa jimbo la Plateau wamesema kuwa, watu waliouawa katika shambulizi hilo i wanaume watano, wanawake wanne na mtoto mmoja. Baada ya hujuma hiyo washambuliaji walitekeleza uharibifu dhidi ya mali za wakazi wa eneo la Daffo, huku wakitoweka baadaye. Polisi ya Nigeria imesema kuwa imeanzisha uchunguzi kwa ajili ya kubaini wahusika wa shambulizi hilo.

Hujuma ya kigaidi Nigeria

Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limekuwa likishuhudia mashambulizi ambayo karibu yote yanafanywa na wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram. Wanachama wa genge hilo walianzisha mashambulizi nchini Nigeria tangu mwaka 2009 ambapo hadi sasa zaidi ya watu elfu 20 wameuawa na wengine milioni mbili na laki sita kuwa wakimbizi. Kushindwa nchi za eneo kukabiliana na harakati za kundi hilo hususan ndani ya Nigeria, kunatajwa kuwa sababu ya kuendelea hujuma za wanachama wa kundi hilo.