Umoja wa Mataifa kuzingatia zaidi ulinzi wa amani barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49185-umoja_wa_mataifa_kuzingatia_zaidi_ulinzi_wa_amani_barani_afrika
Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu amesema, Baraza la Usalama la umoja huo litatilia maanani kazi za mijadala kuhusu ushirikiano wa pande kadhaa na ulinzi wa amani barani Afrika mwezi huu, ambao China inashika uenyekiti wa zamu wa baraza hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 02, 2018 02:30 UTC
  • Umoja wa Mataifa kuzingatia zaidi ulinzi wa amani barani Afrika

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu amesema, Baraza la Usalama la umoja huo litatilia maanani kazi za mijadala kuhusu ushirikiano wa pande kadhaa na ulinzi wa amani barani Afrika mwezi huu, ambao China inashika uenyekiti wa zamu wa baraza hilo.

Amesema kutafanyika jitihada maalumu za kuimarisha uwezo wa oparsheni za kulinda amani za Umoja wa Afrika ili kudumisha usalama katika bara hilo. Amesema hivi sasa iparesheni tano kubwa zaidi za kulinda amani za Umoja wa Mataifa ziko barani Afrika.

Balozi Ma amesema dunia inakabiliwa na changamoto kubwa katika hali ya usalama wa kimataifa. Wakati huohuo, kanuni za kimataifa na ushirikiano wa pande kadhaa unakuwa dhaifu siku hadi siku.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia

Pia amesema Baraza la Usalama ambalo lina majukumu ya msingi kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa, linatakiwa kutoa mchango wa uongozi katika kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi na mifumo ya usalama wa pamoja.