-
Iran yataka UN na nchi wanachama zikatae “ugaidi wa kiuchumi” wa Marekani
Aug 27, 2026 04:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi wanachama wa umoja huo kukataa kampeni mpya ya Marekani ya ugaidi wa kiuchumi dhidi ya Iran, akisema Washington inalenga kuzilazimisha nchi nyingine kuacha mahusiano halali ya kiuchumi na Tehran kwa kutumia vitisho vya vikwazo.
-
Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Vita dhidi ya Iran vimefichua mapungufu ya mataifa makubwa
Aug 25, 2026 11:28Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema kwamba uvamizi wa kijeshi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel dhidi ya Iran umefichua mapungufu ya udhibiti wa madola makubwa, na kuashiria mabadiliko ya uhakika na yasiyoweza kurekebishwa kuelekea mfumo wa kimataifa wa kambi nyingi.
-
Katibu Mkuu wa UN: Hatua kali zaidi zichukuliwe kukomesha ubaguzi kwa sababu ya dini
Aug 23, 2026 03:24Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua zaidi kukomesha vurugu na ubaguzi dhidi ya watu kwa sababu ya dini au imani yao, akionya kuwa mashambulizi dhidi ya jumuiya za kidini ni shambulio dhidi ya haki za binadamu na utu wa binadamu.
-
Katika kumbukumbu ya mwaka wa 81 tangu US ilipoishambulia Hiroshima, UN yataka silaha za nyuklia ziangamizwe
Aug 07, 2026 12:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameonya kuwa dunia inakabiliwa na ongezeko la hatari ya matumizi ya silaha za nyuklia kutokana na kushamiri migawanyiko ya kisiasa, kutokuaminiana na mashindano ya kijeshi.
-
Baghaei amhoji Guterres; kwa nini unahepa kuwataja wavurugaji wawili wakuu wa sheria za kimataifa?
Jul 31, 2026 03:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria matamshi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupuuzwa kwa sheria za kimataifa kwa namna inayotisha, na kumhutubu yeye kwa kumwambia: "Sasa ni wakati wa kutimiza jukumu lako zito na kusaidia kuzuia Umoja wa Mataifa na mfumo wa kanuni zake kutofikwa na hatima ya Jumuiya ya Mataifa."
-
Iravani: Kutochukua hatua UN kunahalalisha haki ya Iran ya kujibu mashambulizi
Jul 19, 2026 03:20Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa umoja huo kufuatia uchokozi wa Marekani dhidi ya Iran, kushambuliwa miundombinu na mauaji ya raia wa Iran.
-
Kamishna wa Haki za Binadamu UN: Mapigano yasitishwe Gaza na Lebanon, aonya kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan
Jun 15, 2026 12:26Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza haja ya kuimarishwa usitishaji mapigano huko Gaza na kufikiwa makubaliano endelevu ya kusitisha mapigano, akibainisha kuwa vikosi vya jeshi la Israel vimewaua Wapalestina wapatao 1,000 tangu usitishaji mapigano Oktoba mwaka jana, pamoja na kuimarisha vizingiti vya kuzuia misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza, jambo ambalo amesema limezidisha mgogoro wa binadamu katika sekta hiyo.
-
Guterres: Wafanyakazi 80 wa Umoja wa Mataifa waliuawa mwaka jana huko Gaza
Jun 09, 2026 11:46Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametangaza kwamba wafanyakazi 136 wa shirika hilo la kimataifa waliuawa wakitekeleza majukumu yao katika mwaka uliopita, wakiwemo wafanyakazi 80 waliokuwa wakifanya kazi katika Ukanda wa Gaza huko Palestina.
-
Balozi wa Iran UN apinga madai ya Marekani kuhusu shambulio dhidi ya kinu cha nyuklia cha UAE
May 24, 2026 03:26Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameyatupilia mbali madai ya Marekani kuhusu shambulio la ndege zisizo na rubani (drone) dhidi ya kinu cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia cha Barakah nchini Falme za Kiarabu (UAE). Amesema kuwa Washington imetumia vibaya Baraza la Usalama ili kusambaza tuhuma za uongo dhidi ya Iran na mpango wake wa nyuklia wenye malengo ya amani.
-
Iran yaiambia UN: Nchi za Ghuba ya Uajemi zinapasa kutoa jibu na kulipa fidia kwa mchango wao katika vita vya Marekani na Israel
May 23, 2026 12:32Amir Saeid Iravani Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi za kusini mwa Ghuba ya Uajemi na Jordan zinabeba dhima ya kuzisaidia Marekani na Israel katika uvamizi wao dhidi ya Iran.