-
China yaitaka Syria iunde serikali shirikishi na ipambane na ugaidi
Mar 26, 2025 07:41Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa mpito wa Syria waandae mchakato wa kuasisi serikali shirikishi na wachukua hatua madhubuti za kupabana na ugaidi nchini humo.
-
Makumi ya wafanyakazi wa UN wanaondoka Gaza, Israel yazidisha mauaji
Mar 26, 2025 02:41Kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya kambi za Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kuuawa wafanyakazi watano wa shirika hilo la kimataifa, makumi ya wafanyakazi wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza wanaondoka eneo hilo kutokana na wasiwasi wa mashambulizi ya Israel.
-
UN, EU zataka kusitishwa vita Gaza huku Israel ikifanya mashambulizi mapya
Mar 22, 2025 04:32Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimetoa wito wa kusitishwa mara moja mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza, huku Israel ikianzisha tena vita vya mauaji ya kimbari kwenye ukanda huo.
-
Iran yakosoa vikali uingiliaji wa nchi za Magharibi katika kazi za Baraza la Haki za Kibinadamu UN
Mar 19, 2025 04:15Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amezikosoa vikali baadhi ya nchi za Magharibi kwa kutumia vibaya taasisi za Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa, nchi hizo zinataka kuingiza siasa katika masuala ya haki za binadamu dhidi ya Iran kwa kupuuza masuala ya kimsingi ya haki za binadamu ukiwemo mgogoro wa Palestina.
-
Guterres ahudhuria futari ya Waislamu Warohingya wa Myanmar kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani
Mar 15, 2025 03:05Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefuturu na wakimbizi wa Rohingya walioko kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox Baazar nchini Bangladesh kuonyesha mshikamano na wakimbizi hao na wenyeji wanaowapa hifadhi.
-
UN: Wakati umefika wa kuunda serikali ya shirikishi nchini Syria
Mar 15, 2025 02:25Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria amesisitiza kuwa, wakati umefika sasa wa kuchukua hatua za dhati na za kijasiri za kuunda serikali ya mpito na ya kuaminika nchini Syria.
-
UN yatoa wito wa kukomeshwa mauaji ya raia nchini Syria
Mar 10, 2025 06:59Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk ameonya katika taarifa yake kuhusu ghasia za hivi karibuni magharibi mwa Syria na kutoa wito wa kukomeshwa mauaji ya raia nchini humo.
-
Siku ya Wanawake; Iran yataka Israel itimuliwe UN + Picha
Mar 09, 2025 06:46Ofisi ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imetaka utawala wa Kizayuni utimuliwe kutoka kwenye umoja huo kutokana na jinai kubwa unazofanya dhidi ya wananchi wa kawaida wa Palestina hasa wanawake na watoto wadogo.
-
Mjumbe wa UN ataka kuimarishwa hadhi ya wanawake nchini Libya
Mar 09, 2025 06:43Hanna Serwaa Tetteh, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ambaye pia ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL ametoa mwito wa kuinuliwa hadhi ya wanawake nchini Libya.
-
UN: Utawala wa Trump uache kuingilia uhuru wa mahakama
Mar 09, 2025 02:38Ripoti Maalumu wa Umoja wa Mataifa amekosoa vikali hatua za hivi majuzi za serikali ya Donald Trump ya kuwatimua na kuwateua maafisa wapya wa mahakama, akielezea wasiwasi wake kwamba hatua hizi ni sehemu ya vitisho kwa uhuru wa mfumo wa mahakama wa Marekani.