UN kujenga ofisi mpya yenye thamani ya dola milioni 340 Nairobi
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubu mjini Nairobi Kenya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amshuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika ofisi yake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika.
Umoja wa Mataifa unasema uwekezaji huo utaifanya Nairobi kuwa moja ya vituo vikuu vya shughuli za kimataifa vya shirika hilo duniani, sambamba na New York, Geneva na Vienna.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres pamoja na Rais wa Kenya William Samoei Ruto wameongoza hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa kituo kipya cha mikutano pamoja na uzinduzi wa majengo mapya ya kisasa katika eneo la Gigiri jijini Nairobi. Akizungumza katika hafla hiyo Guterres amesema
Mradi huo unajumuisha majengo mapya yanayohimili mabadiliko ya tabianchi, ofisi za kisasa pamoja na ukumbi mkubwa wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua wajumbe 1,600 kwa wakati mmoja. Idadi ya vyumba vya mikutano itaongezeka kutoka 14 hadi 30 huku uwezo wa jumla wa wajumbe ukiongezeka kutoka watu 2,000 hadi 9,000.
Makao ya Umoja wa Mataifa Nairobi yanajengwa katika eneo la ekari 140 lililotolewa na serikali ya Kenya, hatua inayotajwa kuwa mchango mkubwa zaidi wa ardhi kuwahi kutolewa kwa Umoja wa Mataifa na nchi mwenyeji.
Guterres yuko mjini Nairobi kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Afrika na Ufaransa ambao umehudhuriwa na viongozi kutoka nchi zaidi ya 30 akiwemo Rais Emannuel Macron wa Ufaransa.