Imarati kujenga Eritrea kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i5314-imarati_kujenga_eritrea_kituo_chake_cha_kwanza_cha_kijeshi_nje_ya_nchi
Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umeanza kujenga kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi huko Eritrea.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 18, 2016 07:29 UTC
  • Imarati kujenga Eritrea kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi

Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umeanza kujenga kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi huko Eritrea.

Taarifa zinasema kuwa picha za satalaiti zilizopatikana zinaashiria kuwepo kituo kimoja kipya cha kijeshi na vile vile kuendelea ujenzi wa bandari katika uwanja wa ndege wa Assab huko Eritrea. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, inaonekana kuwa Imarati hivi sasa inajenga bandari hiyo mpya pembeni ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Assab huko Eritrea, ambayo inaweza kuwa kituo cha kudumu wa kijeshi cha nchi hiyo nje ya Imarati. Picha hizo za satalaiti zinaonyesha kwenda kasi kwa ujenzi huo ulioanza baada ya mwezi Septemba mwaka jana. Eritrea ni nchi inayopatikana katika pwani ya bahari Nyekundu kaskazini mashariki mwa Afrika huku lango la kistratejia la Babul Mandab likiwa njia ya mawasiliano ya baharini kati ya nchi hiyo na Yemen.