HRW yaikosoa Kenya kwa kushindwa kukabiliana na ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i74924-hrw_yaikosoa_kenya_kwa_kushindwa_kukabiliana_na_ongezeko_la_unyanyasaji_wa_kijinsia
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeilaumu serikali ya Kenya kwa kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na ongezeko la vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vilivyojiri wakati wa maambukizi ya corona hususan wakati wa utekelezaji wa zuio la kusalia majumbani ili kuzuia maambukizi ya COVID-19.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 21, 2021 23:52 UTC
  • HRW yaikosoa Kenya kwa kushindwa kukabiliana na ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeilaumu serikali ya Kenya kwa kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na ongezeko la vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vilivyojiri wakati wa maambukizi ya corona hususan wakati wa utekelezaji wa zuio la kusalia majumbani ili kuzuia maambukizi ya COVID-19.

HRW imedai katika ripoti yake ya jana Jumanne kwamba serikali ya Kenya imeshindwa kuhakikisha kuwa wanawake wanapata huduma za kiafya, kiuchumi na za kijamii kufuatia vizuizi mbalimbali vilivyowekwa ambavyo vimeathiri shughuli zao.

Ripoti inasema kulikuwapo ongezeko kubwa la asilimia 301 ya simu zilizoripoti unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana katika wiki mbili za kwanza za kurantini kati ya mwexzi Machi na Aprili 2020.

HRW imesema, wakati tafiti za awali zilionyesha kuwa visa vya unyanyasaji wa kijinsia  vinaongezeka wakati wa dharura za kiafya, serikali ya Kenya inapaswa kutarajia na kubuni mpango sawa wa wakati wa dharura ya afya wa wakati wa ugonjwa wa COVID-19.

Shirika hilo limeongeza kuwa, utafiti mwingine juu ya unyanyasaji wa kijinsia pia umeonyesha kuwa miundo na sera za sasa za serikali ya Kenya "hazitoshi kutoa suluhisho la ukatili dhidi ya wanawake na wasichana" wakati wa dharura kama hizo.

HRW: Unyanyanyasaji wa kijinsia dhid ya wanawake umeongezeka Kenya wakati wa corona

Ripoti hiyo ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch imechapishwa kwa kutegemea mahojiano 26 yaliyofanywa kati ya mwezi Juni mwaka jana na Februari mwaka huu ambapo watu 13 waliohojiwa ni manusura wa unyanyasaji wa kijinsia. HRW limetaja aina mbalimbali za unyanyasaji huo wa kijinsia dhidi ya wanawake na mabinti kama kubakwa, kupigwa, kufukuzwa nyumbani, kulazimishwa kuolewa na kuwalazimisha kukeketwa.