Vikosi vya RSF viyawateka nyara wanajeshi wa Sudan zaidi ya 300
(last modified Wed, 14 Jun 2023 07:50:14 GMT )
Jun 14, 2023 07:50 UTC
  • Vikosi vya RSF viyawateka nyara wanajeshi wa Sudan zaidi ya 300

Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan (RSF) vimewateka nyara askari wa jeshi la nchi hiyo katika jimbo la Darfur Kusini.

Taariifa iliyotolewa na Vikosi vya RSF imesema kuwa vikosi hivyo vimeteka magari 24 ya Land Cruiser na  manne ya deraya yaliyokuwa katika kambi ya jeshi kwenye eneo la mpakani la Umm Dafuq katika jimbo la Darfur Kusini na kuwateka nyara wanajeshi 300 wa jeshi la Sudan. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, raia wanne wa Sudan waliuawa jana katika mapigano kati ya jeshi la SUdan na RSF mjini Khartoum. Nyumba nne pia ziliharibiwa kikamilifu na raia kadhaa wamejeruhiwa. 

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya RSF yalianza tena Jumamosi asubuhi baada ya kumalizika usitishaji vita wa siku moja kati ya pande mbili hizo; na jana mji mkuu Khartoum, Umdurman na maeneo mengine kadhaa yalikumbwa na mapigano na ghasia kati ya pande mbili hasimu. 

Pendekezo la kusimamisha mapigano huko Sudan lilitolewa ili kufanikisha ugawaji wa misaada ya kibinadamu kwa wahitaji. 

Watu zaidi ya 1,800 wameuawa katika mapigano huko Sudan hadi sasa na Umoja wa Mataiaf umetangaza kuwa raia zaidi ya milioni moja wamekuwa wakimbizi ndani ya nchi hiyo mbali na Wasudan laki tatu waliokimbilia nchi jirani kwa ajili ya hifadhi. 

Wakimbizi wa Sudan 

 

Tags