-
Upotoshaji wa Rais wa Ufaransa kuhusu ukoloni barani Afrika
Nov 22, 2022 22:59Katika hali ambayo jinai za Ufaransa katika mataifa mbalimbali barani Afrika zinaendelea kushuhudiwa; Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametahadharisha kuhusiana na satwa na upenyaji wa madola makubwa ya dunia barani Afrika.
-
Kuongezeka watoto wa Kipalestina katika magereza ya Israel
Nov 22, 2022 07:09Wizara ya Mateka na Wafungwa wa Kipalestina Walioachiliwa Huru kutoka gerezani imetangaza kuwa, hivi sasa kuna watoto 170 wa Kipalestina katika magereza ya Israel huku watano kati yao wakishikiliwa pasi na kuelezwa tuhuma na makosa yao.
-
Bin Salman na Bin Zayed hawana ubavu isipokuwa wa kuua watoto wa Kiyemen
Nov 21, 2022 22:53Kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo faili la jinai za kivita la Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na Sheikh Muhammad bin Zayed Al-Nahyan Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) huko nchini Yemen linavyozidi kuwa kubwa.
-
Sisitizo la kuchunguzwa jinai za jeshi la Marekani nchini Afghanistan
Nov 21, 2022 07:23Sambamba na kuanza uchunguzi kuhusiana na jinai za kivita nchini Afghanistan unaofanywa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito wa kuchunguzwa mashambulio ya mauaji ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.
-
Kashfa mpya ya haki binadamu ya serikali ya Marekani
Nov 20, 2022 22:59Wizara ya Mahakama ya Marekani imetoa hukumu ya kuishauri serikali ya nchi hiyo kumtoa kwenye hatia Mohamed bin Salman, mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia katika jinai ya mauaji ya kikatili ya Jamal Khashoggi, mwandishi Msaudia aliyekuwa anaukosoa utawala wa nchi hiyo. Khashoggi aliuliwa kinyama kwa kukatwa vipande vipande na maajenti wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki.
-
Kuongezeka maradufu watu wanaokatwa vichwa nchini Saudi Arabia
Nov 20, 2022 05:18Serikali ya Saudia inatumia vibaya kimya cha madola makubwa na jamii ya kimataifa, kuzidisha kukata vichwa watu kwa visingizio tofauti kiasi kwamba, idadi ya watu waliotekelezewa adhabu ya kifo na ukoo wa Aal Saud mwaka huu, tayari hivi sasa ni maradufu ya waliokatwa vichwa mwaka jana nchini humo.
-
Sweden yathibitisha: Bomba la gesi la Nord Stream liliharibiwa kwa makusudi, vita vya nishati vyapamba moto
Nov 19, 2022 23:05Tangu kuanza kwa vita vya Ukraine, mahusiano kati ya Russia na nchi za Magharibi yameambatana na mizozo na mivutano mingi, haswa katika sekta ya nishati, kwa kadiri kwamba usafirishaji wa gesi kupitia bomba kuu la usafirishaji wa gesi kutoka Russia kwenda Ulaya lijulikanalo kama "Nord Stream", umesimamishwa kwa miezi kadhaa iliyopita kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uvujaji wa gesi.
-
Russia na China zapinga azimio la Bodi ya Magavana ya Wakala wa IAEA dhidi ya Iran
Nov 19, 2022 08:22Azimio jipya la Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani limepasishwa ambapo limetuma ujumbe ulio wazi kufuatia kupungua kwa kura za nchi zilizoliunga mkono licha ya mashinikizo mapya ya kisiasa ya Marekani na Troika ya Ulaya dhidi ya Iran.
-
Hujuma tatu za kigaidi katika kipindi cha wiki tatu Iran; adui anatumia ugaidi baada ya kupoteza matumiani katika vita vya kisaikolojia
Nov 18, 2022 22:58Katika wiki tatu zilizopita, mashambulizi matatu ya kigaidi yametekelezwa Shiraz, Isfahan na Izeh, miji mitatu ya Iran, ambapo raia 24, ikiwa ni pamoja na wanawake kadhaa na watoto, wameuawa shahidi na makumi ya watu wengine kujeruhiwa.
-
Matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula na mkwamo wa kisiasa nchini Marekani
Nov 18, 2022 06:02Hatimaye, baada ya siku 9 za uchaguzi wa Marekani wa katikati ya muhula, kulingana na matokeo yaliyotangazwa ya uchaguzi wa Bunge la Kongresi, chama cha upinzani cha Republican kimepata wingi wa viti katika Baraza la Wawakilishi, nacho chama tawala cha Democratic kikapata wingi wa viti katika Baraza la Seneti.