Hamas: Kitendo cha utawala wa Kizayuni kukataa kukabidhi miili ya mashahidi wa Kipalestina kinaonyesha ukatili
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i130074-hamas_kitendo_cha_utawala_wa_kizayuni_kukataa_kukabidhi_miili_ya_mashahidi_wa_kipalestina_kinaonyesha_ukatili
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeashiria kuwa, utawala ghasibu wa Israel umekataa kukabidhi maiti 726 za mashahidi wa Kipalestina na kukitaja kitendo hicho kuwa jinai na ukatili wa kutisha wa adui Mzayuni.
(last modified 2025-08-27T12:51:17+00:00 )
Aug 27, 2025 12:49 UTC
  • Hamas: Kitendo cha utawala wa Kizayuni kukataa kukabidhi miili ya mashahidi wa Kipalestina kinaonyesha ukatili

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeashiria kuwa, utawala ghasibu wa Israel umekataa kukabidhi maiti 726 za mashahidi wa Kipalestina na kukitaja kitendo hicho kuwa jinai na ukatili wa kutisha wa adui Mzayuni.

Harakati ya Hamas siku ya Jumatano imetangaza kuwa: "Kunyakuliwa miili ya mashahidi wa Kipalestina na adui Mzayuni ni jinai ya kutisha na ya kusikitisha inayothibitisha ukatili wake." Hamas imeongeza: "Tunataka jamii ya kimataifa ichukue hatua za haraka kwa ajili ya kuufedhehesha utawala huu ghasibu na kutumia mbinu zote zilizopo kwa ajili ya kuushinikiza urejeshe miili ya mashahidi wetu."