Apr 01, 2024 04:37 UTC
  • Rais Raisi ahimiza kutekelezwa kivitendo mafundisho ya Qur'ani Tukufu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuzingatia mafundisho wa Qur'ani Tukufu katika nyuga zote ni jambo la dharura kwa ajili ya mafanikio ya wanadamu ya duniani na Akhera.

Sayyid Ebrahim Raisi amenukuliwa na shirika la habari la IRIB akisema hayo hapa Tehran na kuongeza kuwa, mafanikio ya mwanadamu ya duniani na Akhera yamo katika kutendea kazi aya na mafundisho ya Qur'ani Tukufu kwani Kitabu hiki kitakatifu kimebeba ujumbe wa uongofu kwa ajili ya ufanisi wa mwanadamu katika zama zote na kwa ajili ya dunia nzima.

Amesema, mambo yote yanaweza kupatiwa ufumbuzi ndani ya Qur'ani Tukufu kwani Kitabu hicho kitakatifu kina majibu ya maswali yote yanayohusu maisha ya mwanadamu, hivyo kuna wajibu wa kufanyika harakati kijihadi katika kuleta ustaarabu unaotokana na mafundisho ya Qur'ani.

Amesema Qur'ani Tukufu imetilia mkazo mno wajibu wa kuweko umoja na mshikamano madhubuti baina ya Waislamu na leo hii siri ya kufanikiwa jukumu hilo ni kushikamana vilivyo na mafundisho yaliyomo kwenye aya za Kitabu hicho Kitakatifu. 

Tags