Rais Pezeshkian: Iran itawafanya wavamizi magaidi kujutia kitendo chao cha uoga
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran itawafanya wavamizi wa magaidi kujutia kitendo chao cha uoga.
Rais Masoud Pezeshkian amesema hayo katika radiamali yake kuhusu mauaji ya mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, Ismail Haniya.
Huku akilaani mauaji ya Ismail Haniyah, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, Masoud Pezieshkian, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani wa Twitter): Mshikamano kati ya mataifa mawili yenye fahari ya Iran na Palestina utakuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali, na njia ya muqawama na kutetea wanaokandamizwa itakuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran italinda ukamilifu ardhi yake, izza, na heshima yake, na wavamizi wa kigaidi watajutia kitendo chao cha woga walichokifanya.
Wakati huo huo, makundi ya muqawama wa Palestina yametoa taarifa ya kuulaani mauaji dhidi ya Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapamabano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).