Kikao cha Baraza la Usalama kuhusu kuuawa kigaidi Shahidi Haniyeh
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i114732-kikao_cha_baraza_la_usalama_kuhusu_kuuawa_kigaidi_shahidi_haniyeh
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza katika kikao cha Baraza la Usalama kuhusu kuuawa kigaidi Shahidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas kuwa nafasi ya Marekani kama mshirika wa kistratijia na muungaji mkono mkuu wa utawala wa Israel katika eneo katika jinai hiyo ya kutisha haipaswi kupuuzwa.
(last modified 2024-08-01T23:06:30+00:00 )
Aug 01, 2024 23:06 UTC
  • Kikao cha Baraza la Usalama kuhusu kuuawa kigaidi Shahidi Haniyeh

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza katika kikao cha Baraza la Usalama kuhusu kuuawa kigaidi Shahidi Ismail Haniyeh Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas kuwa nafasi ya Marekani kama mshirika wa kistratijia na muungaji mkono mkuu wa utawala wa Israel katika eneo katika jinai hiyo ya kutisha haipaswi kupuuzwa.

Hii ni kwa sababu hatua hii isingechukuliwa bila ya idhini na usaidizi wa kijasusi wa Marekani. 

Katika kikao hicho cha Baraza la Usalama la UN kilichojaidli hali ya mambo katika eneo la Asia Magharibi, Balozi Amir Saeid Iravani ameongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani kitendo hicho kiovu na cha kigaidi kwa nguvu zote na inakichukulia kuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, Hati ya Umoja wa Mataifa na ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala na usalama wa taifa la Iran.

Kitendo cha kigaidi cha utawala wa Kizayuni cha kumuua shahidi Haniyeh ambacho kimelaaniwa na nchi mbalimbali duniani hakuna shaka kuwa utawala wa Kizayuni haukuwa na uwezo wa kutekeleza oparesheni hiyo ya kigaidi hapa Tehran bila ya msaada wa kiintelijensia na kijeshi wa Washington, bali ni wazi kuwa uliogopa taathira zake kali. 

Amin Farhan mchambuzi wa masuala ya kisiasa anazungumzia hili akisema: "Himaya na uungaji mkono huo wa pande zote wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni ndio unaomfanya Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu mtendaji jinai wa utawala huo aachiwe kama mbwa mwenye kichaa katika eneo na hivyo kufanya kila uovu na jinai anazotaka huku wanaomuunga mkkono pia wakiendelea kumhami kwa kiburi. 

Kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni ni kukiuka pakubwa amani na usalama katika eneo na duniani kwa ujumla; na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapasa kuchukua hatua za haraka na athirifu kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa hati ya umoja huo. Wakati huo huo hata kama nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimelaani  katika kikao chao cha dharura kuuliwa kigaidi Ismail Haniyeh hapa Tehran, mauaji yaliyofanywa na Israel, lakini kikao hicho kimeshindwa kuchukua uamuzi madhubuti ili kuzuia kukaririwa kukiukwa mamlaka za kujitawala za nchi mbalimbali kunakofanywa na utawala unaotenda jinai wa Israel bali kimebainisha tu wasiwasi wake katika uwanja huo. 

Hii ni katika hali ambayo ilitazamiwa kuwa kushiriki wawakilishi wa China na Russia nchi ambazo ni wanachamam wa kudumu wa Baraza la Usalama kungepelekea kuchukuliwa uamuzi mkali ili kuzuia kuendelea kukaririwa hujuma za kigaidi za utawala wa Kizayuni katika eneo. Hii ni kwa sababu kuu iliyowapelekea wanachama wa Baraza la Usalama ghairi ya waungaji mkono wa utawala huo kulaani kuuawa shahidi Haniyeh ilikuwa ni kutumbukia hatarini amani na uthabiti wa Asia Magharibi. Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa ametaja kuuawa kigaidi Ismail Haniyeh kuwa ni njama za wazi kwa lengo ka kuvuruga juhudi za amani katika  eneo. 

 

Amar Bendjama, Balozi wa Algeria katika UN 

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa pia amelaani kuuawa shahidi Haniyeh na kusema: 'Yeyote aliye nyuma na waliotekeleza mauaji haya lazima wafahamu namna vitendo hivyo vinaweza kuwa hatari kwa amani ya kimataifa.'

Balozi na Mwakilishi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa pia amesema katika kikao hicho cha Baraza la Usalama kuwa hilo halikuwa shambulio rahisi bali kitendo cha kidhalimu na cha kukiuka mamlaka ya kitaifa ya kujitawala nchi. Amesema, hilo halikuwa shambulio kwa binadamu tu, bali lilikuwa shambulizo ovu dhidi ya uhusiano wa kidiplomasia na kanuni na misingi ya mfumo wa ulimwengu. Ameongeza kuwa jinai ambayo Israel imeifanya imekiuka mamlaka ya kitaifa ya Iran. 

Hata hivyo  Balozi na Naibu Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kwa kiburi ameunga mkono kitendo hicho cha kigaidi cha utawala wa Kizayuni na kusema Marekani haikufahamu lolote kuhusu mauaji ya Ismaill Haniyeh na haikuhusika katika oparesheni hiyo. Balozi na Naibu Mwakilishi wa Marekani katika UN ameeleza haya katika kuendelea sera za uungaji mkono za Washington kwa Israel.  

Naye Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza ameunga mkono waziwazi jinai ya utawala wa Kizayuni ya kumuuwa kigaidi shahidi Haniyeh. Kwa hiyo, ni wazi kabisa kwamba maadamu waungaji mkono wa kile kinachotajwa kama kutetea haki za binadamu wanaendelea kuunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni, utawala huo haramu kwa kiburi na wazi wazi utaendelea kukiuka mamlaka za kitaifa za nchi mbalimbali na kukanyaga sheria za kimataifa; ambapo taathira za vitendo hivyo viovu ni kuitumbukiza hatarini amani na usalama wa dunia. 

Hata hivyo kama alivyosisitiza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Tehran imeazimia kulipiza kisasi cha damu ya mgeni wake mpendwa. Ni dhahir shahir kuwa Marekani na nchi nyingine zinazohami na kuunga mkono utawala wa Kizayuni ndizo zinazopasa kubeba dhima za taathira za kushtadi pakubwa mivutano ya aina yoyote katika eneo. 

Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu