Kan'ani Chafi: Iran yalaani shambulizi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mogadishu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i114858-kan'ani_chafi_iran_yalaani_shambulizi_la_kigaidi_la_al_shabaab_mjini_mogadishu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kan’ani amelaani vikali shambulio la kundi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mogadishu na kuomboleza na serikali ya Somalia na familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi.
(last modified 2024-08-05T04:12:33+00:00 )
Aug 05, 2024 04:12 UTC
  • Kan'ani Chafi: Iran yalaani shambulizi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mogadishu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kan’ani amelaani vikali shambulio la kundi la kigaidi la Al-Shabaab mjini Mogadishu na kuomboleza na serikali ya Somalia na familia za wahanga wa shambulio hilo la kigaidi.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Kan’ani alilaani vikali shambulizi hilo la hivi karibuni la kigaidi katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu.

Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran  pia alitoa pole na rambirambi kwa watu na serikali ya Somalia, akiwahurumia wahanga wa tukio hilo baya na la kinyama lenye kusikitisha kwa mauaji hayo mabaya yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Watu 37 wameuawa katika shambulio la Al-Shabaab katika ufuo wa Mogadishu

Takriban raia 32 waliuawa na wengine 63 kujeruhiwa katika mlipuko kwenye ufuo maarufu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu Ijumaa iliyopita. Polisi na serikali wanalilaumu kundi la kigaidi la al Shabaab kwa shambulio hilo la kigaidi.

Shambulio hilo la kigaidi lilikuwa shambulio baya zaidi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika tangu kulipuliwa mabomu mawili kwenye magari karibu na makutano ya soko lenye shughuli nyingi Oktoba 2022,  ambapo takriban watu 100 waliuawa na wengine 300 kujeruhiwa.

Kundi la kigaidi la Al-Shabaab lilidhibiti eneo kubwa la Somalia kabla ya kurudishwa nyuma katika mashambulizi ya serikali mwaka 2022. Hata hivyo, wanamgambo hao bado wana uwezo wa kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya maeneo ya serikali, kibiashara na kijeshi.