Trump amsifu shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani
(last modified Tue, 15 Oct 2024 12:12:59 GMT )
Oct 15, 2024 12:12 UTC
  • Trump amsifu shahidi  Luteni Jenerali Qassem Soleimani

Rais wa zamani wa Marekani na mgombeaji wa uchaguzi ujao wa rais wa nchi hiyo amesema kuwa, Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyeuawa shahidi, kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha IRGC, alikuwa jenerali mkubwa sana wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Trump, rais wa zamani wa Marekani, ambaye aliamuru kuuawa kwa Luteni Jenerali Qasem Soleimani, kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Januari 2020, siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu wa Marekani, amekiri nafasi muhimu aliyokuwa nayo Jenerali Soleimani.

Trump vile vile amedai kuwa wakati wa urais wake huko Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya  Iran haikuthubutu kushambulia vikosi vya Marekani, na kwamba,  licha ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani kuwa jenerali mkubwa wa Iran, lakini hakuwahi kushambulia vikosi vya Marekani.

Rais huyo wa zamani wa Marekani ameashiria kudorora kwa hali ya nchi hiyo duniani na kusisitiza kuwa inazidi kudidimia siku hadi siku.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran IRGC,  Abu Mahdi Al-Muhandis kamanda wa Hashd Al Shaabi ya Iraq waliua shahidi pamoja na wenzao wengine 8 katika shambulio la anga la wavamizi na vikosi vya kigaidi vya Marekani kwenye Uwanja wa Ndege wa Baghdad, Januari tarehe  3, 2020.

Tags