Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: BRICS inakuwa kambi mpya duniani
(last modified Wed, 23 Oct 2024 10:23:57 GMT )
Oct 23, 2024 10:23 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: BRICS inakuwa kambi mpya duniani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kundi la BRICS linabadilika na kuwa kambi mpya duniani.

Abbas Araqchi ameeleza kuwa kundi la BRICS polepole linakuwa kambi mpya duniani. 

Araqchi ameongeza kuwa: Hivi sasa karibu nchi 30 zinataka kujiunga na kundi hilo.  

Kundi la nchi zinazoibukia kiuchumi zinazojulikana kwa jina la BRICS lilianzishwa mwaka 2006 na Brazil, China, India na Russia; na katika miaka iliyofuata, Afrika Kusini, Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)na Ethiopia hatua kwa hatua zilijiunga na kundi hilo. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ilijiunga rasmi na BRICS kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu. 

Nchi wanachama wa kundi la BRICS 

Nchi wanachama wa kundi la BRICS zinaunda asilimia 45.2 yajamii ya watu wote duniani na asilimia 36.7 ya Pato la Taifa. 

Kulingana na wataalamu, kufikia mwaka 2050 nchi wanachama wa BRICS zitadhamini angalau nusu ya mzunguko wa uzalishaji wa nishati duniani.