Iran yatahadharisha kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya maeneo yake ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135002-iran_yatahadharisha_kuhusu_vitisho_vya_marekani_dhidi_ya_maeneo_yake_ya_nyuklia
Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa mjini Geneva, Uswisi ametahadharisha kuwa hatua ya Marekani ya kuhalalisha vitisho dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii ianahatarisha itibari na hadhi ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).
(last modified 2026-01-01T08:52:06+00:00 )
Jan 01, 2026 08:52 UTC
  • Iran yaonya kuhusu vitisho vya Marekani
    Iran yaonya kuhusu vitisho vya Marekani

Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa mjini Geneva, Uswisi ametahadharisha kuwa hatua ya Marekani ya kuhalalisha vitisho dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii ianahatarisha itibari na hadhi ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Ofisi ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran mjini Geneva imemwandikia barua Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa IAEA na kusema, vitisho vya Marekani dhidi ya miradi ya nyuklia ya Tehran inayofanyika kwa malengo ya amani, vitakuwa na taathira hasi kwa mfumo wa kimataifa unaopiga marufuku usambazji na uenezaji wa silaha za nyuklia.

Ofisi hiyo imesisitiza umuhimu wa kulaaniwa hatua hatarishi kama hizo na kuwawajibsha kikamilifu wale wote wanaosababisha uchochezi. 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, huko Florida siku ya Jumatatu, Rais wa Marekani, Donald Trump alitishia "kutokomeza" jaribio lolote la Tehran la kuendeleza mpango wake wa nyuklia au kuimarisha uwezo wake wa makombora ya balistiki.

Trump alidai kuwa anatumai Iran haitajaribu kujiimarisha tena kwa sababu ikifanya hivyo Marekani haitakuwa na chaguo isipokuwa kuisambaratisha haraka Iran. 

Jumanne wiki hii Rais Masoud Pezeshkian wa Iran alijibu matamshi hay ya Trump na kuahidi kuwa uchokozi wowote dhidi ya Iran utakabiliwa na jibu kali na kumfanya audi ajutie.