Rais Pezeshkian: Umoja utawafanya Waislamu kuwa na nguvu kubwa
(last modified Fri, 01 Nov 2024 02:27:01 GMT )
Nov 01, 2024 02:27 UTC
  • Rais Pezeshkian: Umoja utawafanya Waislamu kuwa na nguvu kubwa

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya umoja baina ya nchi za Kiislamu na kusema: Iwapo tutaweza kufikia umoja katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii, tunaweza kuwa nguvu kubwa katika eneo la Asia Magharibi, na katika hali hii Marekani haiwezi kutuwekea vikwazo.

Daktari Masoud Pezeshkian amesema hayo katika mazungumzo yake na Ayatullah Sayyid Mussa Shobeiri Zanjani mmoja wa wanazuoni na Marajii Taqlid katika mji  Qom, kusini mwa Tehran na kubainisha kwamba, katika mazungumzo yake na viongozi wa eneo, moja mada zilizoibuliwa ni kwa nini Waislamu wanahitafiliana namna hii katika hali ambayo, Wazungu, pamoja na tofauti zao, wameondoa mipaka kati yao na kuwa na sarafu moja.

Rais Pezeshkiana amehoji kwa nini Waislamu wasiwe na umoja na kukumbusha kwamba: Iwapo Waislamu wangeweka kando tofauti zao, utawala wa Kizayuni haungeweza kusababisha maafa haya kwa watu wa Palestina na Lebanon.

Katika safari yake hapo jana katika mji wa Qom, Rais Pezeshkian mbali na kufanya ziara katika Haram ya Fatima Maasuma (as), amekutana pia na Marajii Taqlidi wengine katika mji huo kama Makarim Shirazi, Ja'far Sobhani, Nouri Hamedani na Javadi Amoli.

Aidha amekutana na kufanya mazungumzo pia na Sayyid Javad Shahristani mwakilishi wa Ayatullah Ali Sistani nchini Iran.

Tags