Araghchi: Wamagharibi wameonyesha nia ya kuanza tena mazungumzo ya nyuklia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi, amesema kuwa hivi sasa nchi za Ulaya zinaonyesha nia ya kuanza tena mazungumzo ya nyuklia na kueleza kuwa: Yumkini mazungumzo hayo yakafanya hivi karibuni.
Sayyid Abbas Araghchi amesema kwamba Tehran iko tayari kwa hali yoyote ile na kwa muda wowote ule na akaongeza kuwa: Njia ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa nyeti na tata katika mwaka ujao, na tumejiandaa kwa mazungumzo hayo.
Kuhusu safari zake za kikanda, Araghchi amesema: Ilikuwa lazima katika mazingira ya baada ya kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah huko Lebanon, kuonyesha uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Muqawama na tunapokuwa na kuwahakikkishia marafiki zetu wa Kambi ya Muqawama na Hizbullah kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaendelea kuunga mkono mapambano na kuhuisha hali ya kujiamini.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema katika eneo la Asia Magharibi, kuna uelewa na wasiwasi wa pamoja kuhusiana na vitisho vya utawala pandikizi wa Israel na kuongeza kuwa : Katika mkutano wa kilele wa nchi za Kiarabu na Kiislamu uliofanyika Riyadh, tuliona jinsi Mohammed bin Salman, mwana mfalme wa Saudi Arabia alivyolaani shambulizi la utawala huo dhidi ya Iran.