Araghchi kushiriki mkutano wa UNAOC nchini Ureno
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i119306-araghchi_kushiriki_mkutano_wa_unaoc_nchini_ureno
Abbas Araghchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anatazamia kuelekea nchini Ureno kushiriki katika mkutano wa 10 wa kimataifa wa Kongamano la Muungano wa Umoja wa Mataifa wa Ustaarabu (UNAOC).
(last modified 2024-11-25T03:51:26+00:00 )
Nov 25, 2024 03:51 UTC
  • Araghchi kushiriki mkutano wa UNAOC nchini Ureno

Abbas Araghchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anatazamia kuelekea nchini Ureno kushiriki katika mkutano wa 10 wa kimataifa wa Kongamano la Muungano wa Umoja wa Mataifa wa Ustaarabu (UNAOC).

Ismail Baqae Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa ziara ya Araghchi nchini Ureno inafanyika kulingana na sera amilifu ya mambo ya nje ya Iran.

Ismail Baqae, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran 

Baqae amesema, ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Ureno inafanyika sambamba na sera ya nje hai na athirifu ya Iran kama nchi mwakilishi wa moja ya staarabu kongwe duniani. 

Ziara hii pia imelenga kushirikiana katika michakato ya kidiplomasia ili kukuza amani kwa mujibu wa maelewano, mazungumzo na mapatano ya kimataifa.