Araghchi: Ugaidi nchini Syria ni tishio kwa eneo zima la Asia Magharibi
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, ugaidi nchini Syria ni tishio kwa eneo zima la Asia Magharibi
Seyyed Abbas Araghchi, amesema hayo alipokuuwa akielezea misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu matukio ya eneo, dunia na uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Misri katika mahojiano maalum na mtandao wa Al-Ghad wa Misri pambezoni mwa Mkutano wa Kilele wa Nchi Zinazoendelea za Kiislamu D-8.
Araghchi ameashiria mpango wa muda mrefu wa Wamarekani na Wazayuni wa kuzidhoofisha na kuzisambaratisha nchi kubwa za Kiislamu sambamba na udhibiti wa utawala ghasibu katika eneo hili na kusisitiza kwamba: Muamlama wa utawala wa Kizayuni wakati wa vita vya Gaza na mauaji ya kimbari ya wanawake, watoto na raia zaidi ya 60,000 wa Gaza na Lebanon na hujuma zake dhidi ya Syria na uharibifu wa miundombinu ya kiulinzi na kiuchumi ya nchi hiyo vinaonyesha kuwa usahihi wa maonyo ya Iran kuhusu tishio la Israel kwa eneo zima.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Irabn ameeleza kuwa, lengo kuu la kuundwa mhimili wa muqawama katika eneo hili ni kupambana na kukabiliana na hujuma na uvamizi wa utawala ghasibu wa Kizayuni wa Palestina na kurejeshwa haki za Wapalestina.