Jibu la Iran kwa propaganda za Marekani na utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i124262-jibu_la_iran_kwa_propaganda_za_marekani_na_utawala_wa_kizayuni
Amir Saeed Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma zisizo na msingi za Marekani dhidi ya Iran na kusema: 'Tuhuma hizi zisizo na msingi kwa mara nyingine tena zinabainisha siasa za uadui za serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.'
(last modified 2025-03-23T03:07:24+00:00 )
Mar 23, 2025 03:07 UTC
  • Jibu la Iran kwa propaganda za Marekani na utawala wa Kizayuni

Amir Saeed Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma zisizo na msingi za Marekani dhidi ya Iran na kusema: 'Tuhuma hizi zisizo na msingi kwa mara nyingine tena zinabainisha siasa za uadui za serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.'

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekanusha tuhuma hizo zisizo na msingi za Marekani na Israel dhidi ya Tehran katika barua aliyoliandikia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kusema katika kikao cha baraza hilo: 'Tutuma hizi si lolote ila ni juhudi zilizopangwa kwa ajili ya kupotosha fikra za waliowengi kimataifa kuhusiana na mauaji ya halaiki, jinai za kivita na maafa makubwa yanayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya watu wa Palestina huko Ghaza.'

Akiashiria propaganda zinazoenezwa na Marekani na utawala wa kibaguzi wa Israel kuwa Iran inaunga mkono ghasia na ugaidi Iravani amesema: Tuhuma hizi zisizo na msingi kwa mara nyingine tena zinabainisha wazi siasa za uadui za serikali ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na zinathibitisha kwamba, Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, chini ya muongozo wa moja kwa moja wa Washington, anapuuza hali halisi ya mambo katika medani na kuendelea kutoa tuhuma za kukaririwa na zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.'

Iravani amesisitiza kuwa: Kila mara anapopata fursa, Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa huligeuza Baraza la Usalama kuwa chombo cha kuendeleza ajenda ya kisiasa ya Washington na kutoa taswira isiyo sahihi kuhusu Iran kwa kudai kuwa ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.

Dorothy Shea, Kaimu Mkuu wa ujumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amekariri tuhuma za hapo awali za maafisa wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: 'Hatuwezi kuivumilia Iran yenye silaha za nyuklia ambayo inatenga bajeti kwa ajili ya kufadhili uharibifu na ugaidi katika eneo na kwingineko.'

Hotuba ya Iravani katika kikao cha Umoja wa Mataifa

Ingawa ustawi wa nyuklia wa Iran unawiana na malengo ya amani, lakini Marekani, washirika wake wa Magharibi na utawala wa Kizayuni wanatumia suala hilo kama kisingizio cha kuituhumu Tehran kuwa inafuatilia malengo ya kijeshi ya nyuklia.

Kinyume na tuhuma hizo zisizo na msingi za Wamagharibi, Iran imefanikiwa pakubwa  kutumia teknolojia ya nyuklia  katika nyanja mbalimbali za amani zikiwemo za uzalishaji umeme, dawa na kilimo.

Licha ya vikwazo vikubwa na visivyo na mfano wake vya Marekani, Tehran imesisitiza kuwa haiko tayari kufanya tena mazungumzo na nchi ambayo inakiuka hadharani makubaliano ya kimataifa.

Iran imesisitiza mara kwa mara msimamo wake wa kimsingi wa kupinga utengenezaji na usambazaji wa silaha za maangamizi ya umati kwa kuzingatia fatwa ya wazi iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika uwanja huo. Kwa msingi huo, Iran imeidhinisha mikataba kadhaa ya kimataifa inayopiga marufuku silaha za maangamizi ya umati ukiwemo Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Silaha za Nyuklia. Pia inasisitiza kupigwa marufu matumizi ya silaha za nyuklia kote duniani.

Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani ambako kuna maana ya kusalimu amri mbele ya matakwa yake ya kibabe. Kwa kutilia maanani kusitasita na kushindwa nchi wanachama wa Ulaya kutekeleza ahadi zao za mapatano ya nyuklia JCPOA, mara tu baada ya Marekani kujiondoa, Iran nayo ililazimika kuchukua hatua tano kwa ajili ya kupunguza taratibu ahadi zake katika mapatano hayo.

Ili kuendeleza mazungumzo na kufikia muafaka, suala muhimu kwa mtazamo wa Iran ni utekelezaji wa majukumu ya upande wa Magharibi, ambayo Wamarekani na Troika ya Ulaya hadi sasa wamekataa kuyatekeleza. Sambamba na uvurugaji huo, propaganda chafu za vyombo vya habari vinavyofungamana na White House pia zimeendelea kuenezwa dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani.

Mafanikio ya nyuklia Iran

Tuhuma nyingine ya viongozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni ambayo imekuwa ikirudiwarudiwa mara kwa mara ni eti uungaji mkono wa Iran kwa makundi yanayotuhumiwa kuwa ni ya kigaidi. Matukio ya hivi karibuni katika eneo yanathibitisha wazi kuwa, waanzilishi na wafadhili wakuu wa makundi ya kigaidi ni Marekani na utawala haramu wa Israel.

Ikiwa kiongozi wa nchi za Magharibi na washirika wake wa Magharibi na Kizayuni, Marekani imetoa uungaji mkono mkubwa kwa magaidi wa kitakfiri wakiwemo wa Daesh na kuwachukulia kuwa chombo kizuri cha kufikia malengo yao haramu katika eneo.

Chanzo na sababu kuu ya kukosekana amani katika eneo hili ni uungaji mkono wa wazi na uliofichika wa Marekani kwa viongozi wa makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama katika nchi za Iraq, Syria na Afghanistan.

Katika upande wa pili, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza uungaji mkono wa kimaanawi kwa makundi ya muqawama na ya kupigania ukombozi wa ardhi, katika kukabiliana na uchochezi wa vita wa Marekani na utawala wa Kizayuni. Kinyume na madai ya watawala wa Marekani, Iran inayachukulia mafanikio ya makundi hayo kuwa yanatokana moja kwa moja na uwezo na imani yao katika uwanja wa vita.