Iran yaionya Israel; Shambulio lolote la kijeshi litajibiwa
Katika ujumbe wa kijasiri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekashifu juhudi za "kinjozi" za Israel za kuishurutisha Tehran na kuonya kwamba, shambulio lolote la kijeshi dhidi ya taifa hili litajibiwa mara moja.
Katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa X, Abbas Araghchi amepuuzilia mbali vitisho vya Israel na kusisitiza kuwa "vipo mbali na uhalisia" huko akionya kwamba, shambulio lolote la kijeshi litakabiliwa na jibu.
"Dhana ya Israel kwamba inaweza kuamuru Iran ifanye kile inachotaka, au isifanye isichokitaka, imejitenga na ukweli, na haifai kupewa jibu," ameeleza Araghchi.
Araghchi amesema kinachoshangaza, hata hivyo, ni jinsi (Benjamin) Netanyahu anavyosema kwa ujasiri kile ambacho Rais (Donald) Trump anaweza na hawezi kufanya katika diplomasia yake na Iran.
Amesema: Kwa urahisi, washirika wa Netanyahu katika timu ya Biden Iliyoshindwa - ambao walishindwa kufikia makubaliano na Iran - wanatilia shaka mazungumzo yetu ya moja kwa moja na utawala wa Trump, na kuyaona kama JCPOA nyingine.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amesisitiza kuwa: Hakuna chaguo la kijeshi, na kwa hakika hakuna ufumbuzi wa kijeshi. Shambulio lolote (dhidi yetu) litajibiwa mara moja.
Rais wa Marekani Donald Trump hivi majuzi alisema kuwa, ana "uhakika mkubwa" kwamba utawala wake utaweza kufikia makubaliano na Iran kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.