Erdogan: Israel haiheshimu ahadi zake, kamwe Uturuki haitaiacha Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i134714-erdogan_israel_haiheshimu_ahadi_zake_kamwe_uturuki_haitaiacha_gaza
Rais wa Uturuki amesema: "Utawala wa Israel hauheshimu wala kufungamana na ahadi zake na unazuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kila mara kwa kutumia visingizio mbalimbali."
(last modified 2026-01-03T13:29:21+00:00 )
Dec 25, 2025 08:13 UTC
  • Erdogan: Israel haiheshimu ahadi zake, kamwe Uturuki haitaiacha Gaza
    Erdogan: Israel haiheshimu ahadi zake, kamwe Uturuki haitaiacha Gaza

Rais wa Uturuki amesema: "Utawala wa Israel hauheshimu wala kufungamana na ahadi zake na unazuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kila mara kwa kutumia visingizio mbalimbali."

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema hayo katika hotuba yake jana Jumatano na kubainisha kwamba, licha ya utekelezaji wa usitishaji mapigano huko Gaza tangu Oktoba 11, matatizo katika maeneo ya makazi ambayo yamegeuzwa kuwa magofu na utawala wa Kizayuni yanaendelea kushuhudiwa.

Erdogan alisisitiza kwamba Israel haitekelezi ahadi zake na inaleta vikwazo na ugumu kila mara katika njia ya misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kwa visingizio vya uwongo. Pia aliahidi kwamba msaada wa Ankara kwa Palestina utaongezeka katika miezi ya Rajab, Sha'ban na Ramadhani, na kwamba kamwe Uturuki haitaiacha Gaza kamwe.