Israel yakasirishwa na kauli ya kumdhalilisha rais wake iliyotolewa na Trump
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i136638-israel_yakasirishwa_na_kauli_ya_kumdhalilisha_rais_wake_iliyotolewa_na_trump
Duru zilizo karibu na rais wa utawala wa kizayuni wa Israel zimeyaelezea matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kumtusi na kumdhalilisha rais wa utawala huo Isaac Herzog kuwa ni uvukaji mistari myekundu.
(last modified 2026-02-15T05:39:07+00:00 )
Feb 15, 2026 03:26 UTC
  • Israel yakasirishwa na kauli ya kumdhalilisha rais wake iliyotolewa na Trump

Duru zilizo karibu na rais wa utawala wa kizayuni wa Israel zimeyaelezea matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kumtusi na kumdhalilisha rais wa utawala huo Isaac Herzog kuwa ni uvukaji mistari myekundu.

Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeripoti kuwa, mivutano imepamba moto ndani ya utawala wa kizayuni wa Israel baada ya Trump kumshambulia kwa maneno Herzog kwa sababu ya kutotoa msamaha kwa Benjamin Netanyahu.

Duru zilizo karibu na Herzog zimesisitiza kwamba rais huyo wa Israel anasubiri kutolewa maelezo ya moja kwa moja ya Netanyahu ili ajue kama matusi hayo aliyotoa Trump yametokana na ombi lake au uhamasishaji wake yeye Netanyahu.

Miongoni mwa watu wa karibu na Herzog, imejengeka imani kwamba Netanyahu alimshawishi na kumhamasisha Trump achukue hatua hiyo ambayo haijawahi kushuhudiwa ya kumshambulia rais huyo wa utawala wa kizayuni kwa matusi ya kudhalilisha baada ya yeye Netanyahu kutofanikiwa kupata msamaha wa rais kuhusiana na kesi kadhaa zinazomkabili.

Watu hao wa karibu na Herzog wanaamini kwamba ikiwa itathibiti kwamba Netanyahu alimchochea Trump amtusi Herzog, huu utakuwa uchokozi na uadui usioweza kukubalika.

Trump alimhutubu rais wa utawala wa kizayuni kwamba anapaswa aone aibu kwa kukataa kutoa msamaha kwa Netanyahu.../