Duru ya nne ya mazungumzo ya Iran na Marekani kufanyika karibuni
(last modified Mon, 28 Apr 2025 11:24:45 GMT )
Apr 28, 2025 11:24 UTC
  • Duru ya nne ya mazungumzo ya Iran na Marekani kufanyika karibuni

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, Ismail Baqaei, amesema kuwa, duru ya nne ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani itafanyika Jumamosi ijayo huko Muscat, Oman.

Baqaei amesema hayo leo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari wa ndani na wa nje na kubainisha kwamba, duru hiyo ya nne ya mazungumzo itafanyika Jumamosi ijayo kwa mujibu wa hatia ya makubaliano ya Oman.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amezungumzia pia mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Palestina akisema: "Kwa bahati mbaya, mauaji hayo ya halaiki yanaendelea kwa kasi kubwa zaidi, na karibu watu 300 wasio na hatia wameuawa shahidi, na tumeshuhudia matukio machungu yanayolenga kuiangamiza Palestina."

Ismail Baqaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran

 

Katika upande mwingine, Baqaei amezungumzia safari ya ujumbe wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki nchini Iran na kusema: "safari ya ujumbe wa kiufundi wa Wakala wa IAEA inakuja kama kamilisho la mazungumzo kati ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA na maafisa wa Iran, na mazungumzo hayo yatakuwa ya kiufundi.

Kuhusiana na suala la kutiwa mbaroni kinyume cha sheria raia wa Iran nchini Ufaransa, Baqaei amesema: "Hii ni moja ya migongano ambayo lazima ifafanuliwe. Naona ni jambo lisilokubalika kuwanyima haki raia kwa sababu tu wanatoa malalamiko, na huku kunahesabiwa kuwa ukiukaji wa viwango vya kimataifa na kushiriki na jinai zinazofanywa katika eneo letu."