Mahdieh Esfandiari Muirani mtetezi wa Palestina aachiliwa huru
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i132336-mahdieh_esfandiari_muirani_mtetezi_wa_palestina_aachiliwa_huru
Mahdieh Esfandiari, mwanaharakati wa Iran anayewaunga mkono watu wa Palestina, ameachiliwa kwa masharti kutoka katika jela ya Ufaransa baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya miezi saba.
(last modified 2025-10-24T05:44:34+00:00 )
Oct 24, 2025 02:54 UTC
  • Mahdih Esfandiari
    Mahdih Esfandiari

Mahdieh Esfandiari, mwanaharakati wa Iran anayewaunga mkono watu wa Palestina, ameachiliwa kwa masharti kutoka katika jela ya Ufaransa baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya miezi saba.

Esfandiari ni mkalimani na mhitimu wa Chuo Kikuu cha Lyon, alikamatwa mapema Machi mwaka huu kutokana na harakati zake za kuiunga mkono Palestina, na kupinga jinai za Wazayuni katika Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa tovuti ya Mizan, Shahin Hazami, mwandishi wa habari wa kujitegemea na mtetezi wa Palestina, aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii kwamba, Mahdieh Esfandiari alikamatwa baada ya kutuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Telegram, akilaani mauaji ya kimbari ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Kesi yake itaanza kusikilizwa katika mahakama ya Ufaransa baada ya takriban miezi mitatu. Raia huyu wa Iran alikuwa gerezani kwa muda wa miezi saba bila kufunguliwa mashtaka hadi wiki mbili zilizopita, wakati gazeti la Ufaransa la Le Monde liliporipoti kwamba angekabiliana na jaji Januari mwaka ujao kwa tuhuma za kuunga mkono ugaidi.

Mara baada ya mwanaharakati huyo kuachiliwa huru, Seyyed Abbas Araqchi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alizungumza naye kwa njia ya simu na kumwambia,  "Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba hatimaye umeachiliwa huru na umesimama kidete katika nafasi yako na ukazungumza kwa uthabiti sana.