Iran yatangaza utayarifu wa kupanua ushirikiano na Afrika katika nyanja za afya na tiba
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i125816-iran_yatangaza_utayarifu_wa_kupanua_ushirikiano_na_afrika_katika_nyanja_za_afya_na_tiba
Mshauri Mkuu wa Waziri wa Afya na Elimu ya Tiba wa Iran ametangaza utayarifu wa sekta ya afya ya Jamhuri ya Kiislamu wa Iran kupanua ushirikiano wa kiuchumi na nchi za Kiafrika.
(last modified 2025-04-30T07:19:56+00:00 )
Apr 30, 2025 07:19 UTC
  • Iran yatangaza utayarifu wa kupanua ushirikiano na Afrika katika nyanja za afya na tiba

Mshauri Mkuu wa Waziri wa Afya na Elimu ya Tiba wa Iran ametangaza utayarifu wa sekta ya afya ya Jamhuri ya Kiislamu wa Iran kupanua ushirikiano wa kiuchumi na nchi za Kiafrika.

Akizungumza katika Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano wa Iran na Afrika unaofanyika mjini Tehran, Ali Jafarian, Mshauri Mwandamizi wa Waziri wa Afya, Tiba na Elimu ya Tiba wa Iran amekaribisha suala la kustawishwa ushirikiano na nchi za Afrika na kueleza uwezo wa kiuchumi wa sekta ya afya ya Iran ikiwa ni pamoja na mfumo wa afya, matibabu, elimu ya tiba, utafiti na teknolojia, dawa na vifaa vya matibabu, maendeleo ya miundombinu ya afya na kadhalika.

Jafarian pia amewatolea wito wanaharakati wa kiuchumi kutoka nchi za Kiafrika kupanua ushirikiano na vyuo vikuu vya elimu ya tiba vya Iran, vituo vya sayansi na utafiti, taasisi za matibabu, kampuni za utengenezaji dawa na vifaa vya matibabu, na kampuni zinazotegemea maarifa.

Mkutano wa Tatu wa Iran an Afrika, Tehran

Mkutano wa Tatu wa Ushirikiano kati ya Iran na Afrika unafanyika Tehran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi hususan katika nyanja za afya.

Wawakilishi kutoka nchi 38 na wajumbe 51 rasmi wa nchi za Afrika wanashiriki katika mkutano huo.