Kumbukumbu ya Haj Qassem na Abu Mahdi al-Muhandis yafanyika Baghdad
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i134976-kumbukumbu_ya_haj_qassem_na_abu_mahdi_al_muhandis_yafanyika_baghdad
Kumbukumbu ya mwaka wa 6 tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashd al Sha'abi imefanyika katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.
(last modified 2026-01-03T13:29:21+00:00 )
Jan 01, 2026 03:04 UTC
  • Kumbukumbu ya Haj Qassem na Abu Mahdi al-Muhandis yafanyika Baghdad
    Kumbukumbu ya Haj Qassem na Abu Mahdi al-Muhandis yafanyika Baghdad

Kumbukumbu ya mwaka wa 6 tangu kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashd al Sha'abi imefanyika katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Hauli hiyo iliyofanyika kwa hima ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Baghdad imehudhuriwa na shakhsia mbalimbali wa kisiasa, Maulamaa na baadhi ya wawakilishi wa mataifa mbalimbali ikiwemo Russia.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, aliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashd al Sha'abi na wanamapambano wengine wanane, wakati alipoelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.