Iran yasisitiza kuwekewa vikwazo vya silaha na kuadhibiwa utawala mtenda jinai
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa, jamii ya kimataifa inapaswa kuacha kutoa kauli tupu na badala yake kuchukua hatua za kivitendo ili kuwapa nafuu watu wa Gaza na kukomesha mauaji ya kimbari.
Ismail Baaqaei amesema kuwa, "Kuwekwa vikwazo vya silaha dhidi ya utawala wa mauaji ya halaiki (Israel) na kuhukumiwa na kuadhibiwa kwa wahalifu hao ni jambo la dharura."
Ismail Baqaei, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni, akiashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni wa Gaza na matumizi yake ya njaa kama silaha dhidi ya wakaazi wa ukanda huu ambao wamezingirwa kwa zaidi ya siku 150 amesema: Wapalestina sambamba na kuuawa kwa silaha kali zaidi za Marekani na Ujerumani, wananyimwa pia chakula na kufa kwa njaa katika hali mbaya kabisa na ya kikatili. Njia za usambazaji wa chakula zimekuwa mitego ya vifo, na wagonjwa wanakufa bila kupata chakula na dawa ...
Msemaji wa Idara ya Kidiplomasia ya Iran ameashiria mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Gaza ambayo yamekuwa yakiendelea kwa takriban miaka miwili hivi na kubainisha kwamba, "yote haya yanafuatia miaka miwili ya kampeni ya ugaidi, mashambulizi ya mabomu na maangamizi makubwa ambayo yamesababisha vifo na kujeruhi zaidi ya watu 200,000 wasio na hatia na kufanya asilimia 90 ya eneo la Ukanda wa Gaza kutokuwa na makazi."