Mwandishi wa Misri: Ayatullah Khamenei ni Kiongozi wa Waislamu wote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25964-mwandishi_wa_misri_ayatullah_khamenei_ni_kiongozi_wa_waislamu_wote
Mwandishi mmoja wa Misri amesema kuwa, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kiongozi wa Waislamu wote duniani.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 05, 2017 04:10 UTC
  • Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
    Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mwandishi mmoja wa Misri amesema kuwa, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kiongozi wa Waislamu wote duniani.

Shirika la habari la RASA limeripoti habari hiyo na kumnukuu al Shahat Shata, mwandishi na mchambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu wa nchini Misri akisema kuwa, Ayatullahil Udhma Khamenei ni muungaji mkono wa Palestina, Iraq, Lebanon, Syria, Yemen na Waislamu wote duniani hivyo anastahiki kuitwa Imam na Kiongozi wa Waislamu wote wa Kishia na Kisuni.

Mwandishi huyo wa Misri ameongeza kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ndiye muungaji mkono pekee wa kweli wa Palestina. Amesema, viongozi wengi wa nchi za Kiarabu wamekubaliana na uwepo wa Israel inayozikalia kwa mabavu ardhi za Waarabu na za Kiislamu hasa za Palestina baada ya vita vya Waarabu na Israel vya mwaka 1973, lakini Iran imesimaam imara na kukataa katakati kuweko nchi iitwayo Israel.

 

Vita hivyo vilivyoanza  tarehe 6 Oktoba 1973 na kumalizika tarehe 26 mwezi huo huo wa Oktoba, 1973, vilipiganwa baina ya Wazayuni na muungano wa nchi za Kiarabu ukiongozwa na Misri na Syria na viliishia kwa kushindwa vibaya nchi za Kiarabu na kutekwa milima ya Golan ya Syria na jangwa la Sinai la Misri. 

Kwa mara ya kwanza Waarabu kupata ushindi dhidi ya Wazayuni ni katika mapambano yanayoendeshwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ambayo imewalazimisha Wazayuni kukimbia kusini mwa Lebanon na hadi leo hii Wazayuni wana hofu kubwa kila wanaposikia tu jina la Hizbullah au majina ya harakati nyingine za mapambano ya Kiislamu kama vile Hamas na Jihadul Islami za Palestina.