Meja Jenerali Salami: Majeshi ya Iran yako tayari kujibu vitisho vya maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i87686-meja_jenerali_salami_majeshi_ya_iran_yako_tayari_kujibu_vitisho_vya_maadui
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Iran ni ya ajabu, yenye kuonyesha nguvu na yenye uwezo wa kumzuia adui huku akisisitiza kuwa: "Vikosi vya kijeshi vya Iran viko tayari kujibu vitisho vya adui."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 01, 2022 06:33 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Majeshi ya Iran yako tayari kujibu vitisho vya maadui

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Iran ni ya ajabu, yenye kuonyesha nguvu na yenye uwezo wa kumzuia adui huku akisisitiza kuwa: "Vikosi vya kijeshi vya Iran viko tayari kujibu vitisho vya adui."

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), leo Alhamisi ameyatembelea Maonyesho ya Ulinzi wa Anga na Kielektroniki ya Wizara ya Ulinzi, ambayo yamefanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha Siku ya Sekta ya Kiuchumi nchini, ambapo ametoa shukurani kwa wataalamu, wanasayansi na wafanyakazi wenye bidii ambao ni waaminifu, wanaojitolea na wanajihadi katika Wizara ya Ulinzi na kusema: "Mafanikio ya sekta ya ulinzi ya Iran ni ya ajabu, yenye kuonyesha nguvu na yenye uwezo wa kumzuia adui kushambulia na kimsingi yanaashiria maendeleo ya kiteknolojia yenye viwango vya kimataifa na hivyo adui hawezi kuchukua hatua yoyote katika uwanja wa ulinzi wa anga."

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa: "Katika uga wa utafiti wa kiulinzi Iran imeziba pengo lililokuwepo baina yake na nchi zilizoendelea kiviwanda."

Ndege ya kivita isiyo na rubani ya Iran aina ya Mohajer 6

Kamanda Mkuu wa IRGC amesisitiza kuwa, licha ya kuwekewa vikwazo, vizingiti, ahadi mbovu na usumbufu wa ajinabi, leo hii kwa kuwategemea vijana wasomi Wairani, uwezo unaostahiki na wa kuheshimika umepatikana.

Mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi na kujihami yanaendelea kutoa indhari kwa madola ya kigeni yanayofanya chochoko dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kadiri Iran inavyopiga hatua kubwa katika sekta hiyo ndivyo maadui wake wanavyozidi kufeli na kudhoofika.