Wafanyabiashara wa nchi 71 duniani wameshiriki maonyesho ya Iran Expo 2023
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i97212-wafanyabiashara_wa_nchi_71_duniani_wameshiriki_maonyesho_ya_iran_expo_2023
Mkuu wa Maonyesho ya Kimataifa ya Iran Expo 2023 amesema maooneysho ya mwaka huu yamevutia idadi kubwa ya wafanyabiashara na kuongeza kuwa: "Wafanyabiashara, maafisa wa biashara wa serikali kutoka nchi 71 za dunia wamesafiri hadi Iran kutembelea mambo kadhaa ambayo yamefanywa."
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
May 11, 2023 01:33 UTC
  • Wafanyabiashara wa nchi 71 duniani wameshiriki maonyesho ya Iran Expo 2023

Mkuu wa Maonyesho ya Kimataifa ya Iran Expo 2023 amesema maooneysho ya mwaka huu yamevutia idadi kubwa ya wafanyabiashara na kuongeza kuwa: "Wafanyabiashara, maafisa wa biashara wa serikali kutoka nchi 71 za dunia wamesafiri hadi Iran kutembelea mambo kadhaa ambayo yamefanywa."

Katika mahojiano na IRNA, "Majid Takbiri" wa makao makuu ya maonyesho ya Iran Expo 2023 amesema kuwa katika siku tatu za maonyesho ya Iran Expo 2023, kumekuwa na washiriki kutoka nchi kama vile China, India, Afghanistan, Pakistan, Russia, Iraq, Mali, Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Takbiri ameongeza kuwa: Maafisa wakuu wa nchi 19 kutoka pande zote za dunia zikiwemo za Ulaya na eneo la Ghuba ya Uajemi wakiwemo mawaziri, naibu mawaziri, wakuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na wakuu wa mashirika ya kibiashara wamekuja Iran kutembelea maonyesho hayo.

Afisa huyo wa maonyesho ya kibiashara ya Iran Expo 2023, ameyataja mahudhurio hayo kuwa mazuri sana na kuongeza kuwa idadi ya washiriki ni zaidi ya ilivyotarajiwa.

Takbiri amesema: Nchi 60 zilikuwa tayari zimetangaza utayarifu wao wa kutembelea maonyesho hayo. Lakini wawakilishi wa nchi 71 wamefika nchini Iran kutembelea maonyesho hayo ya mashirika ya Iran ambayo yanataka kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi.

Huku akiashiria kuwa, masuala ya  diplomasia ya uchumi yamekuwa miongoni mwa vipaumbele vya serikali ya 13 ya Iran tangu kuanza kwa kazi yake, mkuu wa makao makuu ya  maonyesho ya Iran Expo 2023 amesema: "Tukio hili kubwa limefanyika katika mwelekeo huu na limeweza kuvutia makampuni 750 ya ndani.

Maonyesho hayo ya 5 ya Uwezo wa Uzalishaji wa Iran yalianza shughuli zake Jumapili iliyopita na kumalizika jana Jumatano.