Raisi: Kuimarisha uchumi ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na vikwazo
(last modified Tue, 13 Jun 2023 12:55:48 GMT )
Jun 13, 2023 12:55 UTC
  • Raisi: Kuimarisha uchumi ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na vikwazo

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuna uwezo mkubwa ambao haujatumika wa kuzidisha mabadilishano ya kiuchumi kati ya Iran na Venezuela na kueleza kuwa, njia ya kutimiza nia ya kufikisha kiwango cha biashara baina ya pande mbili kwenye dola bilioni 20 ni kuimarisha uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

Sayyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo katika kikao cha pamoja cha wafanyabiashara wa Iran na Venezuela mjini Caracas. Amesisitiza kuwa kuimarishwa ushirikiano wa kielimu ni miongoni mwa mambo muhimu katika uwanja wa uchumi na kusema kuna udharura wa kanzishwa ofisi ya masuala ya teknolojia nchini Venezuela.

Raisi amesema kubatilisha vikwazo vya adui na kupata nguvu za kiuchumi ndio njia ya bora zaidi ya kukabiliana na vikwazo hivyo na kusisitiza kuwa: Vijana wa Iran wamebadilisha vikwao hivyo na kuvifanya fursa kupitia njia ya makampuni ya elimu na teknolojia na kuweza kuifikisha Iran katika bara ya amani na utulivu.

Ameutaja uhusiano wa Tehran na Caracas kuwa ni nzuri sana na kutoa wito wa kuondolewa vizuizi vyote katika njia ya mabadilishano ya kiuchumi.

hapo awali akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Caracas, Rais Ebrahim Raisi alisema, mabadilishano ya kibiashara baina ya Iran na Venezuela miaka miwili iliyopita yalikuwa na thamani ya dola milioni 600, na kwamba hivi sasa kiwango hicho kimefikia dola bilioni 3, lakini kitaongezwa hadi dola bilioni 10 katika awamu ya kwanza.

Sayyid Ebrahim Raisi jana Jumatatu alianza ziara rasmi ya kuzitembelea nchi tatu za Amerika ya Latini za Venezuela, Nicaragua na Cuba akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran. 

Tags