-
Kadhaa wauawa katika shambulio la droni kusini ya Sudan
May 16, 2025 07:06Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa huku wengine wengine wakijeruhiwa, baada ya ndege isiyo na rubani kushambulia hospitali moja katika mji wa El-Obeid, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Kaskazini kusini mwa Sudan jana Alkhamisi.
-
Trump azitaka kampuni za US zitengeneze droni kama za Iran
May 16, 2025 07:01Rais wa Marekani, Donald Trump amesema ameziomba kampuni za Marekani kutengeneza ndege zisizo na rubani zinazofanana na droni za Iran, ambazo si ghali sana bali zina kasi ya juu na hatari.
-
Ansarullah: Iran imetekeleza wajibu wake wa Kiislamu kuiunga mkono Palestina
May 16, 2025 06:52Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameipongeza Iran kwa uungaji mkono wake usio na kikomo kwa taifa la Palestina na kadhia yao halali na kueleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inafuata njia ya heshima katika suala hilo na nchi nyingine zote za Kiislamu lazima zifuate mkondo huo.
-
NATO inayoongozwa na Marekani yakumbwa na sakata la ufisadi
May 16, 2025 06:48Imefichuka kuwa, nchi nyingi duniani zimeanzisha uchunguzi wa rushwa katika mfumo wa ununuzi wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) linaloongozwa na Marekani.
-
Watoto nusu milioni waingia hatarini kutoka na ghasia mjini Tripoli Libya
May 16, 2025 02:22Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema kuwa, kuongezeka ghasia ndani na karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli, kunatishia usalama wa karibu watoto nusu milioni mjini humo.
-
Rais wa zamani wa Mauritania aongezewa kifungo, sasa ni miaka 15 jela
May 16, 2025 02:21Mahakama ya rufaa ya Mauritania imemhukumu rais wa zamani wa nchi hiyo, Mohamed Ould Abdel Aziz kifungo cha miaka 15 jela kwa tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha.
-
Hamas: Maisha ya mateka wa Israel si muhimu kwa Netanyahu
May 16, 2025 02:21Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetilia mkazo masharti yake makuu kuhusu makubaliano ya kudumu ya kusimamisha vita na kuondoka kikamilifu wanajeshi vamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ikitangaza kuwa, Netanyahu amefeli katika njama zake za kufikia makubaliano bila ya kusitisha vita kikamilifu na kwamba mateka wa Kizayuni si muhimu kwa Netanyahu.
-
Ukidhabi mkubwa wa Israel kuhusu mashambulizi yake dhidi ya hospitali za Ghaza wafichuka
May 16, 2025 02:20Gazeti moja la lugha ya Kiebrania limefichua kwamba jeshi la Israel lilitoa taarifa za uongo kuhusu kuwepo handaki la Hamas chini ya "Hospitali ya Ulaya" (The European Hospital) huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Ghaza, na kwamba hospitali hiyo ililengwa na mashambulizi makubwa ya mabomu mara mbili ndani ya saa 24 bila ya kuweko handaki lolote la HAMAS.
-
DRC yatishia kuweka vikwazo vikali zaidi vya mauzo ya madini adimu ya cobalt
May 16, 2025 02:18Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kuwa inaweza kuweka vikwazo vikali zaidi vya mauzo ya cobalt wakati marufuku yake ya miezi minne itakapomalizika.
-
Kwa nini utawala wa Kizayuni ni utawala wa mauaji ya kizazi?
May 16, 2025 02:16Sisitizo la Israel la kuendeleza vita Gaza katika mwezi wake wa ishirini na kuendelea kuwaua kwa umati wakazi wa ukanda huo hususan wanawake na watoto si tu kwamba kumeibua mijadala ya upinzani na kulaaniwa kimataifa kitendo hicho, bali hata nchi za Ulaya zimekuwa zikiukosoa utawala huo ghasibu kwa hatua zake hizo za kikatili.