-
Je, BRICS Itazuia Vipi Siasa na Hatua za Upande Mmoja za Marekani?
Sep 13, 2026 10:22Mkutano wa 18 wa kilele wa BRICS mjini New Delhi unafanyika wakati ambapo kundi hilo si tena kama muungano wa kiuchumi wa mataifa yanayoinukia pekee; bali, limebadilika kuwa jukwaa muhimu la mashindano kuhusu sura ya baadaye ya mfumo wa dunia.
-
Shambulio la Marekani dhidi ya Meli za Mafuta za Iran: Mvutano Wahama kutoka Shinikizo la Kiuchumi hadi Mapigano ya Kijeshi
Sep 13, 2026 09:22Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kupitia taarifa kuwa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayatasita kutumia haki yake ya kimsingi ya kujilinda kisheria na kwamba yatajibu vikali na ipaswavyo kitendo chochote cha uchokozi wa kijeshi wa adui.
-
Kwa nini Marekani Inahusisha Mgogoro wa Yemen na Iran?
Sep 13, 2026 09:19Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa madai ya uongo ya Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, hayawezi kubadili uhalisia wa mambo kwamba Ansarallah ya Yemen ni kundi huru linalofanya maamuzi yake lenyewe, halipokei maagizo kutoka kwa mtu yeyote wala kufanya kazi kama kibaraka wa upande mwingine.
-
Rais wa Iran: Tunahitaji mageuzi ya kweli katika mifumo ya kimataifa
Sep 13, 2026 07:23Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa suala la utawala na mamlaka shirikishi ya dunia na kuimarishwa mfumo wa pande nyingi lina umuhimu mkubwa zaidi hivi sasa.
-
Iran: mkutano wa Oman ni hatua muhimu kuelekea utulivu na usalama wa kikanda
Sep 13, 2026 07:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, mkutano uliopangwa kufanyika nchini Oman Jumatatu ya kesho utakuwa hatua muhimu kuelekea kuhakikisha utulivu na usalama katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Mufti wa Oman: Umma wa Kiislamu umekumbwa na fitina kubwa
Sep 13, 2026 07:20Mufti wa Oman, Sheikh Ahmed Al-Khalili, amekosoa misimamo ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu kuhusu Ansarullah ya Yemen, akieleza kuwa, hali imekuwa ya hatari kutokana na kuzuka tena mapigano nchini humo.
-
Mlipuko wa Ebola DRC wavuka kiwango cha wagonjwa 7,000 na kuenea hadi mkoa wa saba
Sep 13, 2026 07:18Ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umevuka kiwango cha wagonjwa 7,000 waliothibitishwa na kufikia mkoa wa saba baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika katika mkoa wa Sud-Ubangi.
-
Niger yateua mkuu mpya wa majeshi baada ya jaribio la uasi lililozimwa
Sep 13, 2026 07:13Serikali ya kijeshi ya Niger imemteua mkuu mpya wa jeshi, kufuatia jaribio la uasi wa jeshi lililozimwa mwezi uliopita. Hayo ni kwa mujibu taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa.
-
Iran: Mlango Bahari wa Hormuz unabaki kwenye udhibiti wetu kamili; dunia iilaumu US kwa kupanda bei ya mafuta
Sep 13, 2026 07:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesisitiza kuwa Mlango wa Bahari wa Hormuz unasalia kuwa chini ya udhibiti kamili wa Iran, akisema Marekani ndiye wa kulaumiwa kwa kuvurugika usalama wa baharini wa eneo hilo na inapasa ilaumiwe pia kwa kupanda bei ya mafuta duniani.
-
Askari wa Israel asema waliambiwa: 'Mnao watu milioni mbili wa kuwalenga shabaha Ghaza'
Sep 13, 2026 07:05Askari wa akiba wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel amesema, maafisa wa jeshi hilo wanaichukulia idadi yote ya Wapalestina milioni mbili wa Ukanda wa Ghaza kama walengwa halali wa kuuawa, na amesimulia mauaji mengi yaliyofanywa na askari wa kizayuni na jinsi utekelezaji wa kanuani za vita ulivyoporomoka wakati wa mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa eneo hilo.